Jumanne, 21 Februari 2017

KESI YA MBOWE YAANZA KUSIKILIZWA LEO MAHAKAMA KUU.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Freeman  Mbowe(kushoto) akiwa Mahakama  Kuu  kwa ajili ya  kupeleka  ombi  la zuio la muda  la kukamatwa na polisi. Katika kesi hiyo jopo la Majaji  wanaoisikiliza wametoa  uamuzi  wa kutokamatwa kwa Mwenyekiti huyo kwa muda,  Aidha; Mahakama Kuu hiyo imemtaka Mwenyekiti huyo kurejea Mahakamani hapo Februari  23, mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wakisubiri taarifa za ombi la zuio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman  Mbowe.
Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Peter Kibatala akitoa maelezo kuhusu ombi hilo, kwa waandishi wa habari. 

Maoni 2 :

  1. Kwa kuwa hiki ni chanzo sahihi kabisa cha habari za Mahakamani mngetuambia kilichoamuliwa na Mahakama zaidi ya picha

    JibuFuta
    Majibu
    1. Ufafanuzi juu ya maamuzi ya kesi hiyo unajieleza katika maelezo ya picha ya kwanza, tafadhali soma vizuri.

      Futa