Ijumaa, 10 Februari 2017

MENEJIMENTI YA MAHAKAMA YA TANZANIA YAMUAGA RASMI NAIBU MSAJILI, MAHAKAMA KUU YA TANZANIA BAADA YA KUSTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA


    Naibu Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Euphemia Mingi (aliyesimama) akipunga mkono kama ishara ya kuwaaga rasmi Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania akiwa anakaribia kuanza likizo ya kustaafu Utumishi wa Mahakama ya Tanzania ambayo ametumikia kwa miaka 41.


Naibu Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Euphemia Mingi (aliyeketi katikati), Kaimu Mwenyekiti wa Menejimenti ya Mahakama ya Tanzania ambaye pia ni Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Sollanus Nyimbi (kulia) na Mkurugenzi wa Mipango, Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Mwangu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama, picha hii imepigwa kama kumbukumbu ya kumuaga rasmi Mjumbe wa Menejimenti ya Mahakama, Mhe. Mingi ambaye anatarajia kustaafu Utumishi wa Mahakama hivi karibuni. Mhe. Mingi amehudhuria katika Kikao cha Menejimenti ya Mahakama kwa mara ya mwisho, Februari 10, 2017 na kutumia fursa hiyo kuwaaga rasmi Wajumbe wa Menejimenti.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni