Alhamisi, 17 Agosti 2017

NAFASI 200 ZA KAZI-TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 200

1.0     Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa  Sheria ya Uendeshaji wa  Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri  watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama.

Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Hakimu Mkazi Daraja la II – (TJS 2) nafasi 100, Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 20, Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – (TGS B) nafasi 45, Mpokezi   – (TGS A) nafasi 1, Dereva Daraja la II – (TGOS A) nafasi 10, Mlinzi (TGOS A) nafasi 21 na Afisa TEHAMA Daraja la II Nafasi 3 (TGS.E).

A.   Hakimu Mkazi  II – TJS 2  - (Nafasi 100)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mahakama katika Mikoa iliyoainishwa katika Jedwali hapa chini:-
NA
KANDA
MKOA
WILAYA
IDADI YA NAFASI
1
ARUSHA
MANYARA
DM HANANG
2

DM SIMANJIRO
2
ARUSHA
DM NGORONGORO
1
2
KILIMANJARO

DM MOSHI
1

DM HAI
1

DM ROMBO
2

DM SAME
1

3

MWANZA
MARA
DM BUNDA
1
DM TARIME
2
DM SERENGETI
3

GEITA
DM GEITA
1
DM CHATO
2
DM BUKOMBE
2
MWANZA
DM SENGEREMA
1
4
MBEYA
MBEYA
DM MBEYA
3
DM KYELA
2
DM ILEJE
1
5
IRINGA
IRINGA
DM KILOLO
2
NJOMBE
DM NJOMBE
1
DM WANGING'OMBE
2
DM MAKETE
1
6
DODOMA
SINGIDA
DM IRAMBA
3
DM MANYONI
3
DM SINGIDA
3
DODMA
DM BAHI
2
DM KONGWA
2
7
TABORA
KIGOMA
DM KIGOMA
2
DM KASULU
3
DM KIBONDO
2
TABORA
DM TABORA
1
DM IGUNGA
1
DM URAMBO
1
8
BUKOBA
KAGERA
DM MULEBA
3
DM NGARA
1
9
TANGA
TANGA
DM PANGANI
2
DM MUHEZA
2
DM KILINDI
1
DM MKINGA
1
10
MTWARA
MTWARA
DM MTWARA
1
DM TANDAHIMBA
1
DM NANYUMBU
1
LINDI
DM LINDI
1
DM KILWA
3
11
SONGEA
RUVUMA
DM NYASA
1
DM TUNDURU
2
DM NAMTUMBO
2
12
SHINYANGA
SIMIYU
DM MASWA
3
DM MEATU
2
DM ITILIMA
1
DM BUSEGA
2
13
SUMBAWANGA
RUKWA
DM SUMBAWANGA
3

DM KALAMBO
4


DM NKASI
3


KATAVI
DM MPANDA
2
DM MLELE
1
JUMLA KUU
100

Sifa za kuingilia:-
Waombaji wawe na Cheti cha kuhitimu kidato cha Nne/Sita, Shahada ya kwanza ya Sheria “Bachelor of Laws” (LLB) kutoka katika Chuo kikuu kunachotambulika na Serikali pamoja na cheti cha mafunzo ya Sheria kwa vitendo (Law school Certificate).

Kazi za kufanya:-
       i.       Kuandaa mpango wa kusikiliza mashauri.
     ii.       Kusikiliza mashauri ya awali ya Jinai (Criminal Cases), Madai (Civil Cases), Mirathi (Probate and Administration) na ndoa (Matrimonial Cases).
    iii.       Kutoa hukumu katika mashauri yote anayoyasikiliza  ya jinai, madai, mirathi, ndoa na mashauri  mengine, kadri sheria inavyomruhusu.
    iv.       Kutoa amri mbalimbali za kimahakama anazoruhusiwa kisheria katika Mahakama za Mwanzo.
     v.       Kusuluhisha mashauri.
    vi.       Kusikiliza rufani kutoka Mabaraza ya Kata.

B.   AFISA TEHAMA  DARAJA II TGS E – (Nafasi 3)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mahakama katika Mikoa iliyoainishwa katika Jedwali hapa chini:-
S/N
KANDA
KITUO
IDADI YA NAFASI
1
DODOMA
MAHAKAMA KUU DODOMA
1
2
SONGEA
MAHAKAMA KUU SONGEA
1
3
DAR ES SALAAM
MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA ARDHI
1
JUMLA KUU
3

Sifa za kuingilia:-
Mhitimu wa Kidato cha nne/sita, na mwenye Stashahada ya juu au Shahada ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo;
Sayansi ya Kompyuta
Teknolojia ya Habari
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Menejimenti ya Mifumo ya Habari au Mafunzo mengine yanayohusiana na fani hii.

Kazi za kufanya:-

Watafanya kazi za “Programming” kama ifuatavyo:-
       (i)        Kuandaa, kuandika na kufanya majaribio ya program (plan code and test program)
      (ii)        Kusahihisha program (Debug Program)
     (iii)        Kuweka na kuhakikisha usalama wa program (Incorporate security setting into program)
     (iv)        Kushirikiana na wadau wengine katika kutengeneza programu mbalimbali (Corporate with other software developers)
      (v)        Kufanya  kazi nyingine atakazopangiwa na mkubwa wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.

C.   KATIBU MAHSUSI  DARAJA III TGS B – (Nafasi 20)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mahakama katika Mikoa iliyoainishwa katika Jedwali hapa chini:-

NA
KANDA
MKOA
WILAYA
IDADI YA NAFASI
1
ARUSHA
ARUSHA
DM KARATU
1
2
MOSHI
KILIMANJARO
RM MOSHI
1
3
MWANZA
MWANZA
RM MWANZA
1
DM ILEMELA
1
MARA
DM MUSOMA
1
GEITA
RM GEITA
1
4
MBEYA
MBEYA
DM MBEYA
1
5
IRINGA
IRINGA
DM KILOLO
1
6
DODOMA
DODMA
DM KONDOA
2
7
TABORA
KIGOMA
DM KIBONDO
1
8
BUKOBA
KAGERA
RM BUKOBA
1
DM KARAGWE
1
9
MTWARA
LINDI
DM LIWALE
1
10
SONGEA
RUVUMA
DM NYASA
1
11
SHINYANGA
SIMIYU
RM SIMIYU
1
12
SUMBAWANGA
RUKWA
RM RUKWA
1
KATAVI
RM KATAVI
1
13
DAR ES SALAAM
MOROGORO
DM MVOMERO
1
PWANI
DM RUFIJI
1

JUMLA KUU
20

Sifa za kuingilia:-
Kuajiriwa  wahitimu  wa kidato cha IV  waliohudhuria  Mafunzo ya Uhazili  na kufaulu  mtihani wa Uhazili  Hatua ya Tatu. 
Wawe wamefaulu  somo la Hatimkato  ya Kiswahili na Kiingereza (Shorthand) maneno 80 kwa dakika moja na  wawe wamepata  mafunzo ya Kompyuta  kutoka chuo chochote kinachotambuliwa  na Serikali na kupata cheti katika programu za  Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail  na Publisher.

Kazi za kufanya:-
Katibu Mahsusi  Daraja la III atapangiwa  kufanya kazi Typing pool  au chini  ya Katibu Mahsusi  mwingine mwenye  cheo cha juu  kumzidi  kwenye ofisi  ya Mkuu wa sehemu au kitengo.

(i)        Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
(ii)      Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanazoweza kushughulikiwa.
(iii)     Kusaidia  kutunza taarifa, kumbukumbu  za matukio, miadi, wageni, tarehe  za vikao  safari za Mkuu wake  na ratiba  ya kazi  zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia  kazi, na kumuarifu Mkuu wake  kwa wakati  unaohitajika.
D.           MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II TGS B – (Nafasi 45)
 Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mahakama katika Mikoa iliyoainishwa katika Jedwali hapa chini:-
NA
KANDA
MKOA
WILAYA
IDADI YA NAFASI
1
ARUSHA
MANYARA
DM SIMANJIRO
2
2
MOSHI
KILIMANJARO
DM SAME
1
DM ROMBO
1
3
MWANZA
MWANZA
DM KWIMBA
2
DM UKEREWE
2
DM MISUNGWI
1
MARA
DM SERENGETI
2
4
MBEYA
MBEYA
DM KYELA
2
DM MBARALI
1
DM MBOZI
1
5
IRINGA
IRINGA
DM KILOLO
2
NJOMBE
DM MAKETE
1
6
DODOMA
DODOMA
DM DODOMA
1
SINGIDA
DM SINGIDA
1
DM MANYONI
1
7
TABORA
TABORA
DM SIKONGE
1
DM URAMBO
1
KIGOMA
DM KIBONDO
1
8
BUKOBA
KAGERA
DM NGARA
1
DM MULEBA
2
DM KARAGWE
1
9
TANGA
TANGA
DM MUHEZA
1
DM MKINGA
1
10
MTWARA
MTWARA
DM NANYUMBU
1
DM NEWALA
1
LINDI
DM NACHINGWEA
1
11
SONGEA
RUVUMA
DM NAMTUMBO
2
DM MBINGA
1
12
SHINYANGA
SHINYANGA
DM KISHAPU
2
13
SUMBAWANGA
RUKWA
DM SUMBAWANGA
1
DM KALAMBO
1
KATAVI
DM MPANDA
1
14
DAR ES SALAAM
MOROGORO
DM KILOMBERO
2
PWANI
DM MAFIA
2
JUMLA
45

Sifa za Kuingilia:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti/Stashahada ya utunzaji kumbukumbu kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma pamoja na wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Diploma ya Sheria kutoka chuo cha Uongozi wa Mahakama.

Kazi za kufanya:-
(i)        Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
(ii)      Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
(iii)     Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka Katia reki (file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
(iv)     Kunukuu (kurekodi) mwenendo mzima wa kesi na kuweka kumbukumbu sahihi za mashauri yanayosikilizwa na Majaji au Mahakimu.
(v)      Kuhakiki na kuandaa taarifa iliyohakikiwa na kuwasilisha sehemu husika kabla yakutoa nakala kwa Umma.
(vi)     Kufanya kazi nyingine za kiutawala zinazohusu masuala ya kimahakama kama kuwasilisha nyaraka za kisheria Mahakamani na kuangalia muda na siku ya kufanyika kwa kesi husika.
(vii)    Kuthibitisha machapisho (transcripts) kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi ndani ya muda uliopangwa.
(viii)  Kutunza na kuhifadhi machapisho (transcripts) mahali salama.
(ix)     Kuratibu utoaji wa machapisho (transcripts).
(x)      Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa. 
E.           MPOKEZI TGS A – (Nafasi – 1)
NA
KANDA
MKOA
KITUO
IDADI YA NAFASI
1
DAR ES SALAAM
DAR ES SALAAM
MAHAKAMA YA RUFANI
1

Sifa za Kuingilia:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati na Kufuzu mafunzo ya mapokezi na upokeaji simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
Kazi za kufanya:-
              (i)          Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao.
             (ii)          Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na Ofisi yake.
           (iii)          Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maafisa mbalimbali Ofisini.
           (iv)          Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
             (v)          Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa nje ya ofisi.
F.            DEREVA DARAJA LA II TGOS A – (Nafasi 10)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mahakama katika Mikoa iliyoainishwa katika Jedwali hapa chini:-
NA
KANDA
MKOA
WILAYA
IDADI YA NAFASI
1
ARUSHA
MANYARA
DM SIMANJIRO
1
2
MWANZA
MWANZA
DM UKEREWE
1
3
IRINGA
NJOMBE
RM NJOMBE
1
4
DODOMA
SINGIDA
DM MANYONI
1
5
BUKOBA
KAGERA
DM NGARA
1
6
MTWARA
MTWARA
DM MTWARA
1
7
SHINYANGA
SHINYANGA
DM KAHAMA
1
8
SUMBAWANGA
RUKWA
DM SUMBAWANGA
1
9
DAR ES SALAAM
MOROGORO
DM KILOSA
1
DM MVOMERO
1

JUMLA
10

Sifa za Kuingilia:-
Kuajiriwa wenye Cheti cha Baraza la mitihani (NACTE) Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II (VETA).
Kazi za kufanya:-
(i)           Kuendesha magari ya abiria, na malori,
(ii)          Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
G.           MLINZI TGOS A – (Nafasi 21)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mahakama katika Mikoa iliyoainishwa katika Jedwali hapa chini:-
NA
KANDA
MKOA
WILAYA
IDADI YA NAFASI
1
ARUSHA
ARUSHA
HC ARUSHA
1
2
MOSHI
KILIMANJARO
DM ROMBO
1
3
MWANZA
MWANZA
DM MAGU
1
MARA
DM TARIME
2
GEITA
RM GEITA
1
4
MBEYA
MBEYA
HC MBEYA
1
5
IRINGA
IRINGA
DM MUFINDI
1
6
DODOMA
SINGIDA
DM IRAMBA
1
7
TABORA
TABORA
DM NZEGA
1
KIGOMA
DM KASULU
1
8
BUKOBA
KAGERA
DM BIHARAMULO
2
9
MTWARA
LINDI
RM LINDI
1
10
SONGEA
RUVUMA
RM SONGEA
1
11
SHINYANGA
SHINYANGA
DM SHINYANGA
1
DM MEATU
1
SIMIYU
DM BUSEGA
1
12
SUMBAWANGA
KATAVI
DM MLELE
1
13
TANGA
TANGA
DM HANDENI
1
14
DAR ES SALAAM
MOROGORO
DM MVOMERO
1
JUMLA
21

Sifa za kuingilia:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/ JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Kazi za kufanya:-
           (i)         Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
             (ii)       Kuhakikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za  uhalali wake.
           (iii)       Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
           (iv)       Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
             (v)       Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wanaidhini ya kufanya hivyo.
           (vi)       Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile moto, mafuriko n.k. na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile polisi na zimamoto.
          (vii)       Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 04/09/2017 saa 9:30 Alasiri.

2.0       Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi
            pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-

-      Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
-      Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).
-      Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
-      Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.

NB.     Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).

3.0   Aidha, inasisitizwa kwamba:-

3.1     Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44
3.2     Waombaji wakazi toka maeneo husika na wenye sifa zilizoainishwa  
           katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi katika
           maeneo husika.
3.3     Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi 
          mwombaji.
3.4     Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao   kwa
           waajiri wao wa sasa.
3.5     Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba 
          waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
3.6     Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa
          Mahakama ya Tanzania.
3.7     Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
3.8     Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
3.9     Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha
           watakazotumia maombi yao.
3.10   Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa 
           Umma.
3.11   Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi
            moja.
3.12   Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia     
           mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao  
           hayatashughulikiwa.

4.0     Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi
          wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM.

Imetolewa na ;-
                                     


Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni