Jumatatu, 14 Juni 2021

AFISA KUMBUKUMBU WA MAHAKAMA KISUTU AFARIKI DUNIA

 TANZIA

Marehemu Julieth Gabriel Chaba enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake, Bi. Julieth Gabriel Chaba (pichani) kilichotokea Juni 11, 2021.

Marehemu Julieth alikuwa akifanya kazi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu-Dar es Salaam kama Afisa Kumbukumbu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mazishi yatafanyika kesho Juni 15, 2021 Maswa Mjini mkoani Simiyu.

Mahakama inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni