Na NOEL DAUDI- Mahakama, Songea
Menejimenti ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, tarehe 18 septemba, 2025 imefanya kikao kutathimini utendaji kazi katika kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kikao hicho kilichofanyika wilayani Tunduru katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Wilaya Tunduru kilifunguliwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele, ambaye alikuwa ni mwenyekiti katika kikao hicho.
Kulikuwa na uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kimahakama kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2025 katika Mahakama Kuu Kanda ya Songea, ambayo iliwasilishwa na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Bw. Allan Mwela ambaye alikuwa ni Katibu katika kikao hicho.
Mtendaji aliwasilisha taarifa hiyo ambayo ilikuwa na masuala mbalimbali ikiwemo utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, ambapo aligusia nguzo namba moja inayohusu utawala na usimamizi wa uendeshaji wa shughuli za Mahakama.
Aidha Mtendaji aliwasilisha pia taarifa nguzo ya tatu ambayo ni kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau kama vile utoaji elimu kwa umma na ushughulikiaji wa malalamiko kwa wakati ili kuboresha taswira ya Mahakama.
Naye Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mhe. Asha Waziri aliwasilisha taarifa nguzo namba mbili inayohusu utoaji wa haki kwa wakati ambayo iligusia masuala ya usimamizi wa mashauri na usimamizi wa mashauri kwa njia ya mtandao (VC).
Mambo mengine ni vikao vya mshauri ya mauaji (criminal sessions), usimamizi masjala ndogo ya Mahakama ya Rufani, upandishaji wa mashauri kwenye mfumo pamoja na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano [TEHAMA].
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni