Jumatano, 29 Mei 2024

JAJI MAGHIMBI: JAJI MLAY AMEACHA ALAMA HAITASAULIKA

 Na Magreth Kinabo- Mahakama

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi amesema marehemu Jaji mstaafu wa Mahakama wa Kuu, Juxon Mlay alikuwa ni mtu  wa haki na maamuzi yake yameacha alama katika sekta ya sheria.

 

Mhe. Jaji Maghimbi alisema kwa niaba ya, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani kwenye Ibada ya kuuga mwili wa  marehemu Jaji Mlay iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Azania  Front, lililoko jijini Dar es Salaam.

 

“Jaji Mlay hakupenda chombo chochote kujibebesha mamlaka, ambayo hakijapewa, hivyo alikuwa ni mtu wa haki ambaye anasisitiza kwa kuzingatia sheria,”alisema Mhe. Jaji Maghimbi.

 

Aliongeza kwamba atakumbukwa kwa maamuzi na miongozo aliyoamua kwa kuwa yataendelea kutumiwa na yameacha alama ambayo haitasahulika.

 

Jaji Maghimbi alisema marehemu alikuwa akipenda kuona amri zinazotolewa na Mahakama zinatekelezwa ipasavyo.

 

Naye Kiongozi wa Ibada hiyo,ambaye ni Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo, Chediel Lwiza alisema marehemu alikuwa ni mcha mungu, huku akisisitiza kwamba kazi ya ujaji, uhakimu na uwakili ni ya mungu na mungu ni wa haki,  hivyo ili kuweza kutimiza wajibu katika kutoa haki ni lazima na mahusiano na mungu.

 

Ibada hiyo ilihudhuriwa na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakamu Kuu,wakiwemo majaji wastaafu, viongozi wa serikali wastaafu na waombelezaji mbalimbali.

 

Marehemu Jaji Mlay alifariki dunia tarehe 25 Mei, 2024, mwili wake utasafirishwa kesho mkoani Kilimanjaro na utazikwa Ijumaa  tarehe 31Mei, 2024 nyumbani kwake Himo.

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi akizungumza  wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa  Jaji mstaafu wa Mahakama wa Kuu, marehemu Juxon Mlay , iliyofanyika leo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Azania  lililoko jijini Dar es Salaam.

 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (aliyeshika maua)akiongoza msafara wa kuingiza mwili wa marehemu kanisani.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Warioba (wa kwanza kulia), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Andrew Chenge(wa pili kulia) wakiwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania,Mhe.  Ferdinand  Wambali wa (pili kushoto), na Dkt. Mary Calorine Levira(wa kwanza kushoto).

 
Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa na baadhi ya ya waombelezaji katika ibada hiyo.

  
Kiongozi wa Ibada hiyo,ambaye ni Msaidizi wa Askofu wa kanisa hilo, Cheje Luiza akizungumza jambo wakati wa ibada hiyo.

  
Familia ya marehemu ikiwa katika ibada.

Waombelezaji wakiwa katika ibada.

 Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania,Mhe.  Dkt. Mary Calorine Levira akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Baadhi ya Majaji wakiubeba mwili wa marehemu.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe Angela Bahati akimpa pole mke marehemu Flora Mlay (aliyevaa mewani).



Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Dkt. Theodora Mwenegoha akisaini katika kitabu cha maombelezo nyumbani kwa marehemu.


Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania  wakiwasili nyumbani kwa Marehemu.



Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania  wakiwa nyumbani kwa Marehemu.

Baadhi ya waombelezaji  wakiwa nyumbani kwa Marehemu.

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni