Ijumaa, 28 Juni 2024

KIKAO CHA MAHAKAMA YA RUFANI KUANZA JULAI MOSI

 Na MAGRETH KINAB0-Mahakama

 

Mahakama ya Rufani Tanzania imepanga kusikiliza mashauri 121 katika kikao kitakachoanza tarehe Mosi Julai, hadi tarehe 19 Julai, 2024, ikiwa ni  hatua ya utekelezaji wa  mpango maalum wa kumaliza mashauri.

 

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kikao cha kutathimini kikao hicho  cha Mahakama ya Rufani, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Mwarija wakati akiongoza kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo mahakamani hapo.

 

Akizungumza leo tarehe 28 Juni, 2024 katika kikao hicho, Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe hao kutoa mawazo yao yatakayowezesha kikao hicho, kama kilivyopangwa.

 

Awali akitoa taarifa ya tathimini ya kikao, Katibu wa kikao hicho cha kutathimini, ambaye pia ni Naibu Msajili wa Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rashid Chaungu alisema tayari maandalizi ya kufanyika kwa kikao hicho, yameshafanyika na taratibu mbalimbali zinaendelea kufanyika ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

 

“Tayari hati za kuitwa shaurini zimesambazwa na bado zinaendelea kusambazwa,” alisema Mhe. Chaungu.

 

Aliongeza kuwa katika  kikao hicho, kutakuwa na mashauri ya rufaa za maombi ya madai, rufaa za jinai, maombi ya jinai, rufaa za madai na Civil reference(marejeo).

 

Chaungu alisema kikao hicho kitakuwa na majopo matatu na kitafanyika Dar es Salaam sanjari na vikao vingine vinavyofanyika katika kanda za Arusha,Musoma, Mwanza na Mbeya na vyote vikiwa ni mwendelezo wa vikao vya Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2024.

 

Akichangia hoja Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Paul Ngwembe alisema mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) hayupo katika kikao hicho na kilichopita, hivyo kuna umuhimu wa kuwasiliana na Rais wa TLS ili waweze kushiriki.

 

Akijibu hoja hiyo Mwenyekiti wa kikao hicho, Mhe. Jaji Mwarija alisema TLS waandikiwe barua.

 

Naye mjumbe wa kikao hicho ambaye ni Mrakibu wa Magereza kutoka Gereza la Segerea, Blandina Mbelwa alisema kuna changamoto ya usafiri na kuomba  suala hilo liweze kupatiwa kipaumbele.

 

Mwenyekiti wa kikao cha kutathimini kikao cha Mahakama ya Rufani Tanzania, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Mwarija(katikati)akiongoza kikao hicho, kilichofanyika  leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo mahakamani hapo, (kushoto )ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rehema Mkuye na (kula) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania,Mhe. Dkt. Gerald Ndika.

 Mwenyekiti wa kikao cha kutathimini kikao cha Mahakama ya Rufani Tanzania, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Mwarija (wa pili kulia walioketi katikati)akiongoza kikao hicho, kilichofanyika  leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo mahakamani hapo.

 Katibu wa kikao cha kutathimini kikao cha Mahakama ya Rufani Tanzania na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rashid Chaungu(kushoto) akisoma taarifa ya kikao hicho, (kulia) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania,Mhe. Rehema Mkuye.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Sam  Rumanyika (aliyenyoosha kidole) akichangia hoja.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe.   Zephrine Galeba (aliyenyoosha mikono) akichangia hoja.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rehema (Kerefu) akichangia hoja.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe, David Ngunyale (wa pili kulia), (wa pili kula) ni Jaji  Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Division ya Biashara, Mhe. Cyprian Mkeha, (wa pili kushoto) (wa kwanza kushoto )ni Jaji  Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Elinaza Luvanda na (wa kwanza kulia ) ni Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Aziza Mbadjo.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka,Nassoro Katuga.


Mrakibu wa Magereza kutoka Gereza la Segerea, Blandina Mbelwa akichangia hoja.

Wajumbe wa kikao hicho.



 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni