Jumanne, 4 Juni 2024

MAAFISA MAHAKAMA 15 MBEYA WANOLEWA

Na Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya

Mahakimu 15 wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Mbeya wanapatiwa mafunzo ya namna bora ya kushughulikia mashauri yanayohusu unyanyasaji kijinsia na kingono ile hali wakihakikisha wanaepuka kutonesha majeraha ya kisaikolojia kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia ‘Avoiding Re-traumatization’

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyoanza jana tarehe 3 Juni, 2024 katika ukumbi wa mikutano Mahakama Kuu Mbeya, Mgeni rasmi ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru amewataka washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu ili wakawe mabalozi wazuri katika kuwasilisha kile ambacho wamekipokea katika mafunzo hayo.

“Natoa wito kwa kila mmoja wenu kushiriki kikamilifu na kushirikiana na wakufunzi wetu ili kuongeza uelewa wetu na ujuzi kwenye eneo la usikilizaji mashauri ya ukatili wa kijinsia” alisema Jaji Ndunguru

Naye, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu aliwakaribisha wakufunzi na washiriki katika mafunzo hayo na kuwaahidi kuwa Ofisi ya Naibu Msajili Kanda ya Mbeya ipo tayari kushirikiana nao kwa changamoto zozote endapo zitajitokeza wawapo hapa Mbeya na kuwataka wajisikie vizuri muda wote wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanawezeshwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa na Naibu Msajili kutoka Masjala Kuu Dodoma Mhe. Mwajabu Mvungi. Mafunzo hayo yameratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) chini ya ufadhili wa Irish Rule of Law International (IRLI)

Mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 3 Juni, 2024 hadi tarehe 5 juni, 2024 katika ukumbi wa Mahakama Kuu Mbeya. 


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Kulia ni aji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa.

Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani)

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa (aliyesimama mbele) akiendelea kutoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa (aliyesimama mbele) akiendelea kutoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa akiendelea kutoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo (hawapo pichani)

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda Mbeya Mhe. Victoria Nongwa akifafanua malengo ya mafunzo hayo kwa washiriki.

Naibu Msajili Mahakama ya Tanzania kutoka Masjala Kuu Dodoma Mhe. Mwajabu Mvungi akitoa mada kwa washiriki wa mafunzo hayo (hawapo pichani)

Afisa ustawi Bi. Eva John akieleza utaalamu wa usaidizi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.

Washiriki wa mafunzo hayo wakipokea elimu kwa vitendo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni