Jumanne, 25 Juni 2024

TANZIA - MTUMISHI WA MAHAKAMA YA MWANZO ILALA DAR ES SALAAM AFARIKI DUNIA

Marehemu Ellen Mashauri Makaranga enzi za uhai wake.

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtumishi wake Bi. Ellen Mashauri Makaranga aliyekuwa akihudumu Mahakama ya Mwanzo Ilala kwa nafasi ya Msaidizi wa Kumbukumbu.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam-Kisutu, Bi. Athanasia Kabuyanja, marehemu Ellen alikutwa na umauti jana tarehe 24 Juni, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo.

Bi. Kabuyanja amesema mipango ya maziko inaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu Kigogo jijini Dar es Salaam.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu mzito wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni