Na HILARI GADIYE HERMAN- Mahakama, Lindi
Mahakama ya Tanzania imemkabidhi Mkandarasi kutoka Kampuni
ya ‘Engineering Plus’ viwanja vitatu
kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miradi mitatu ya Mahakama za Mwanzo mkoani Lindi.
Miradi hiyo itakayogharimu jumla ya shilingi Bilioni
3.5 za kitanzania inajumuisha mradi
wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi, Mahakama ya
Mwanzo Mtandi iliyoko Wilaya ya Kilwa na Mahakama ya Mwanzo Ndomoni iliyopo Wilaya
ya Nachingwea.
Akizungumza wakati wa makabidhiano miradi hayo hivi
karibuni Mhandisi Mshauri Bw. Berno
Batinamani alisema, ujenzi wa miradi ya Mahakama hizo tatu utachukua muda
wa miezi sita (6) kwa mujibu wa mkataba hadi kukamilika kwake. Miradi hiyo
unatarajiwa kuanza kutekelezwa kuanzia tarehe 13 Julai 2024 na kukamilika mnamo
tarehe 12 Januari, 2025.
Aidha, Bw.Batinamani
alitoa wito kwa Viongozi wa Vijiji vyote watakao nufaika na miradi
hiyo kumpatia ushirikiano Mkandarasi huyo anayetekeleza ujenzi wa miradi hiyo ili
aweze kuikamilisha kwa wakati. Aliongeza kuwa, miradi hiyo ni fursa kwa wanachi
kwani nguvu kazi itahitajika wakati wa ujenzi wa miradi hiyo hivyo itawanufaisha
kiuchumi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Lindi Bi.Quip Godfrey Mbeyela aliahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa pande
zote zinazohusika na miradi hiyo, huku akiwataka Mhandisi Mshauri, Mkandarasi
na viongozi wote wafanye kazi kama timu moja ili zoezi la ujenzi likamilike kwa wakati.
Naye, Mkadiriaji Majenzi kutoka Mahakama ya Tanzania
Bw. Abdallah Nalicho alimtaka
Mkandarasi kukamilisha kazi kwa wakati na kufuata vipengele vyote vilivyo
ainishwa kwenye mkataba.
Nao, wananchi pamoja na viongozi kutoka vijiji
vilivyonufaika na mradi wa ujenzi wa Mahakama hizo wamefurahishwa sana na
miradi hiyo na kukiri kwamba miradi hiyo itawaondolea adha ya kufuata huduma za
kimahakama umbali mrefu na kuongeza kuwa miradi hiyo itakuwa chachu ya
maendeleo katika maeneo yao.
Makabidhiano ya miradi hiyo yalifanyika kati ya
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Qiup Godfrey Mbeyela na
mwakilishi kutoka Kampuni ya ujenzi ya E-Plus Mhandisi Silas Paul huku yakishuhudiwa na Mkadiriaji
Majenzi wa Mahakama Bw. Abdallah
Nalicho, Mhandisi kutoka Mahakama Bw. Kelvin Juvinal na Mhandisi Mshauri
Bw.
Berno Batinamani kutoka Kampuni ya Norman.
Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering Plus’ Mhandisi Silas Paul akionyeshwa mipaka na Mkadiriaji Majenzi wa Mahakama ya Tanzania Bw. Abdallah Nalicho (Aliyevalia reflector)
Makabidhiano ya Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa
Mahakama tatu za mwanzo Lindi kati ya Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering
Plus’ Mhandisi Silas Paul na Mtendaji wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip
Godfrey Mbeyela.
Makabidhiano ya Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa
Mahakama tatu za mwanzo Lindi kati ya Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering
Plus’ Mhandisi Silas Paul na Mtendaji wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip
Godfrey Mbeyela
Makabidhiano ya Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa
Mahakama tatu za mwanzo Lindi kati ya Mkandarasi kutoka kampuni ya ‘Engineering
Plus’ Mhandisi Silas Paul na Mtendaji wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip
Godfrey Mbeyela
Mwenyekiti wa kikao cha makabidhiano ya eneo la mradi
Bw. Berno Batinamani (aliyenyoosha mkono) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa mipaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni