Jumatano, 28 Agosti 2024

UGENI KUTOKA MAHKAMA KUU ZANZIBAR KATIKA PICHA

Na SALUM TAWAN-Mahakama, Dar es Salaam

Katikati ni Msajili Mkuu wa Mahakma ya Tanzania Mhe. Eva Kiaki Nkya na kulia wa kwanza ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri  Mhe. Desderi Kamugisha wakiwa katika majadiliano ya pamoja na Watumishi wa Mahkama Kuu Zanzibar (waliopo kushoto) waliokuja kwa ajili ya kujifunza mambo yanayohusu usimamizi wa mashauri.

Kulia ni Msajili Mkuu wa Mahkama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, pembeni yake wa kwanza kushoto ni Bw. Said Hemed Khalfani ambae ni Mkuu wa Kitengo cha Mashauri Mahakama Kuu Zanzibar akiwa na wadau wengine kutoka Mahakama Kuu Zanzibar waliokuja kujifunza mambo muhimu yanayohusu usimamizi wa mashauri.

Kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, pembeni yake ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri, Mhe. Desderi Kamugisha  a wa kwanza kulia ni Mhe. Agnes Mchome wakiwa katika majadiliano ya pamoja na watumishi kutoka Mahkama Kuu Zanzibar kuhusu mafunzo yanayohusu usimamizi wa mashauri.

Kushoto ni Bw. Ramadhani Omar Ali ambae ni Afisa Sheria Msaidizi wa Mahkama Kuu Zanzibar, katikati ni Naibu Mrajis Mahakama Kuu Zanzibar, Mhe. Faraji Shomari Juma na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mashauri Mahkama Kuu Zanzibar Bw. Said Hemed Khalfan.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni