SALAAM ZA POLE
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, amesikitishwa na taarifa ya kifo cha Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Serikali na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fredrick Mwita Werema kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam jana tarehe 30 Desemba, 2024 alipokuwa akipatiwa matibabu.
Anatoa pole kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari, Majaji, Familia, ndugu, jamaa na marafiki.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni