Alhamisi, 26 Desemba 2024

KITUO JUMUISHI CHA MASUALA YA FAMILIA TEMEKE CHAKABIDHIWA GARI MPYA YA MAHAKAMA INAYOTEMBEA

Na NAOMI KITONKA, IJC- Temeke

Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke kinachoshughulikia masuala ya Mirathi, Ndoa na Familia kimekabidhiwa gari mpya na ya kisasa ya Mahakama Inayotembea (Mobile Court Services).

Gari hiyo ilikabidhiwa tarehe 23 Desemba, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Moses Ndelwa kwa Mtendaji wa Mahakama ya Kituo hicho, Bw. Samson Mashalla akiwa pamoja na Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mhe. Mwamini Kazema, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo, Mhe. Aloyce Mwageni pamoja na Afisa Tawala wa Kituo hicho, Bi. Doris Arika.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Gari hiyo, Mhe.  Ndelwa alisema, “tunatambua umuhimu wa mashauri yanayosimamiwa na Mahakama hii hivyo, tunawaongezea nguvu kazi kwa kuwapatia gari hii mpya ili kufanikisha upatikanaji wa huduma za kimahakama katika mitaa ya wananchi wetu.”

Akitoa neno la shukrani Mtendaji wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Bw. Mashalla alishukuru kwa kupokea gari hilo jipya la Huduma za Kimahakama Mtaani (Mobile Court Services) ambapo alikiri kuwa, litachangia upatikanaji haki kwa haraka kwa asilimia kubwa na kuendelea kuwafikia wananchi wasioweza kufika mahakamani kudai haki zao.

Zoezi la mapokezi ya Gari hilo liliambatana na zoezi la kusaini fomu za uhakiki wa vifaa vilivyopo katika gari hilo pamoja na Madereva kukabidhiana. 

Muonekano wa gari jipya la Mahakama Inayotembea lililokabidhiwa hivi karibuni kutoa huduma katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke.

Mtendaji wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Temeke akisaini fomu ya uhakiki wa vifaa vivavyopatikana katika gari jipya la Mahakama Inayotembea lililokabidhiwa kituoni hapo hivi karibuni.

Kaimu Naibu Msajili wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwamini Kazema (mbele) akikabidhiwa karatasi ya   makabidhiano kwa ajili ya uhakiki wa vifaa kituoni hapo.

Muonekano wa ndani wa gari jipya la Mahakama Inayotembea  lililokabidhiwa katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke.

Baadhi ya vifaa vinavyopatikana ndani ya gari jipya la Mahakama Inayotembea lililokabidhiwa katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke.
 
Mtendaji wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Bw. Samson Mashalla akiwa katika picha ya pamoja na Karani wa Mahakama Inayotembea, Bi. Mwahija Aziz wakati wa makabidhiano ya gari hiyo kituoni hapo.

Naibu Msajili kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania, Mhe. Ndelwa (aliyesimama Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Bw. Samson Mashalla (wa pili kushoto), 
Kaimu Naibu Msajili wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwamini Kazema (wa pili kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo-Temeke, Mhe. Aloyce Mwageni (wa kwanza kushoto) na Afisa Tawala wa Mahakama hiyo, Bi. Doris Arika (wa kwanza kulia) wakati wa makabidhiano ya gari jipya la Mahakama Inayotembea kituoni hapo.

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni