Na HABIBA MBARUKU-Mahakama, Dodoma
Wajumbe wa Bodi ya Rufaa za Mapato ya Kodi Tanzania
(Tanzania Revenue Appeals Board-TRAB) leo tarehe 26 Agosti, 2026 wametembelea
Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania ili kujifunza kwa vitendo jinsi mifumo
mbalimbali ya Mahakama, hususan Mfumo wa Kielektronki wa Usimamamizi wa
Mashauri (e-CMS) inavyofanya kazi.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uelewa wa namna mifumo
ya Mahakama kwenye utoaji haki inavyotekeleza majukumu yake kwa kutumia
teknolojia za kisasa.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Richard Kabate, pamoja na Wataalamu wa TEHAMA wa Mahakama, walieleza kwa
vitendo namna mfumo wa e-CMS wa Mahakama unavyofanya kazi zake za kusimamia
mashauri katika ngazi mbalimbali za Mahakama.
Wajumbe hao walipata fursa ya kuuliza maswali kuhusu
mfumo huo, na baadaye kutembelea Chumba Maalumu cha Usimamizi wa Taarifa za
Mahakama (Judiciary Situation Room) pamoja na Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call
Centre).
Ugeni huo uliongozwa na Mwenyekiti Msaidizi wa TRAB, huku Wajumbe wengine wakiwa Katibu Mtendaji wa TRAB, Mkurugenzi wa Sheria wa TRAB, Maofisa kutoka Wizara ya Fedha pamoja na wengine.
Naibu Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Richard
Kabate, akitoa wasilisho kwa Menejimenti, Wajumbe wa Bodi ya Rufaa za Mapato ya
Kodi Tanzania pamoja na Maofisa kutoka Wizara ya Fedha namna Mfumo wa Kielektronki
wa Usimamamizi wa Mashauri unavyofanya kazi leo tarehe 26 Agosti, 2026, Makao
Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa
Sheria wa Bodi ya Rufaa za Mapato ya Kodi Tanzania, Bi. Sekela Mwabukusi
akisikiliza wasilisho kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Richard Kabeta (hayupo pichani).
Katibu Mtendaji
Bodi ya Rufaa za Mapato ya Kodi Tanzania, Bi. Bahati Ndoserua, akisikiliza
wasilisho.
Menejiment na Wajumbe wa Bodi ya Rufaa za Mapato ya
Kodi Tanzania wakifuatilia maelekezo ya namna Mahakama inavyofuatilia mwenendo
wa shughuli zake kupitia Chumba Maalumu cha Usimamizi wa Taarifa za Mahakama
(Judiciary Situation Room).
Picha ya pamoja
ya Menejiment, Wajumbe wa TRAB na Watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania,
walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha Mahakama ya
Tanzania.
Picha nyingine ya pamoja ikijumuisha Menejiment, Wajumbe wa Bodi ya Rufaa za Mapato ya Kodi Tanzania na Watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania baada ya kumaliza ziara yao Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania.
Picha ya Meza Kuu, kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Richard Kabate, na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Rufaa za Mapato ya Kodi Tanzania, Bw. Christopher David.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni