Ijumaa, 16 Juni 2017

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AMEWATAKA WANASHERIA KUTUMIA UZOEFU KISHERIA KUPITIA VITABU VYA ZANZIBAR.




Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma,(wa pili kulia ) akiwa katika  picha  ya  mara baada ya kukabidhiwa  seti ya vitabu  vitano  vya sheria kutoka pamoja  na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee  Haji( wa pili kushoto) kwa Niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar(ambaye hayupo pichani) na wa kwanza kulia  ni Mkuu wa Kitengo cha Uandishi wa Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mumarak.

Na  Magreth Kinabo.

Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania, Mhe. Profesa  Ibrahim  Juma, amewataka  wanasheria  wa Tanzania Bara kujifunza  uzoefu  wa kubadilisha sheria mbalimbali  kwa kutumia vitabu   vya sheria  kutoka Zanzibar kwa ajili ya kufanya utafiti na kufundisha katika vyuo vikuu.

Kauli hiyo imetolewa  leo tarehe 16.06.2017,   na Kaimu Jaji Mkuu huyo, wageni kutoka Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, wakati akizungumza  na ujumbe huo mara   baada kuwasili katika Ofisi  ya Mahakama ya Rufani Tanzania, iliyopo jijini  Dar es kwa ajili  mazungumzo ya kubadilisha uzoefu juu ya mabadiliko  ya vifungu vya  sheria mbalimbali.

Ugeni huo, ulikabidhi seti ya vitabu vitano vilivyobadilishwa kutoka 35, ambapo ulizungumzia kuhusu mabadiliko hayo na masuala mbalimbali ya Mahakama ya Tanzania.

“Kuna  haja ya kujifunza sheria bora kutoka Zanzibar, ambazo zinaweza kusaidia kufanya tafiti mbalimbali na kutumika kufundisha kwenye vyuo vikuu.,” alisema Mhe. Jaji Mkuu.

Aidha  Mhe. Jaji  Kaimu Jaji Mkuu huyo aliushukuru ugeni huo, kwa kukabidhi vitabu hivyo kwa niaba ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,Mhe. Omar Makungu.

Akizungumzia kuhusu vitabu hivyo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Mzee Haji alisema  vitabu hivyo vilivyokabidhiwa  ni mabadiliko kutoka vitabu vya sheria 35 hadi vitano. Mabadiliko hayo ya kisheria yamefanyika kutoka mwaka 1980 hadi 2015.
Mhe. Mzee alisema ofisi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano na kubadilisha uzoefu wa masuala hayo na mengine ya  Mahakama baina ya pande  zote mbili .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni