Jumatano, 31 Januari 2018

PROFESA KABUDI: BADO MAHAKAMA ZINATAJIKA KUJENGWA


 Na Magreth Kinabo
Waziri wa Katiba  na Sheria, Profesa  amesema  kwamba  bado changamoto  ya uhitaji mkubwa ujenzi na  ukarabati miundombinu ya Mahakama nchini.

Kauli hiyo ilitolewa leo na wakati akizindua wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, iliyopo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya mkakati wa  Mahakama wa kukabiliana na  changamoto hiyo.

“ Ni ukweli usiopingika  kuwa tuna  changamoto kubwa  ya miundombinu ya Mahakama  hapa nchini. Hadi  kufikia mwaka  jana tulikuwa  tunahitaji  kujenga Mahakama  kuu  19, Mahakama  Hakimu Mkazi  14, Mahakama za Wilaya 109 na mahakama za mwanzo 3003’’, alisema Waziri huyo.

Aliongeza kwamba  tukio hilo  linampa  faraja  kwa kuwa  linatatua moja ya changamoto kubwa inayoikabili Mahakama  na Sekta ya Sheria  kwa  ujumla.

 Profesa Kabudi alifafanua kwamba katika  hali iliyopo ya mahitaji makubwa ya ujenzi na ukarabati wa Mahakama  nchini ubunifu, umakini na kuweka vipaumbele  katika kujikwamua  na hali iliyopo.

 Hata hivyo Profesa Kabudi aliupongeza uongozi wa Mahakama  kwa kuwa wabunifu na kufanya tafiti ya teknolojia  ya gharama  nafuu katika ujenzi  iitayo  Moladi  kwa ajili ya kutumia na kujengea majengo ya Mahakama,

“Nimetembelea  majengo haya ya mahakama nimeridhishwa na viwango vya ubora majengo haya. Teknolojia  hii  sio tu  inapunguza gharama  za ujenzi, bali  pia inapunguza muda wa ujenzi.  Faida hizo  zinawezesha fedha nyingine kutumika katika kujenga au kukarabati majengo mengine,” alisisitiza.

Alisema Serikali inatambua  jukumu la kutenda haki haliwezi kuwa la ufanisi pasipo miundombinu ya kisasa na inayokidhi vigezo vya eneo husika.

Alitoa  wito kwa  Mahakama kuendelea kushauriana na Serikali ili tuweze kufikia  malengo tuliyojiwekea ya kupanua  wigo wa upatikanaji wa haki kwa kujenga na kukarabati Mahakama  zetu.
Aidha  Profesa  aliwata watumishi  na watumiaji wa mahakama hiyo kuitunza miundombinu waliojengewa  ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Kwa upande  wake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu  aliutaka uongozi wa wilaya hiyo uanze kufikiria  eneo lingine la ujenzi wa mahakama  nyingine.


Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni pamoja na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni.
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni

 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza kabla ya kuzindua Mahakama mpya ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Mahakama. Kulia kwake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na kushoto kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akifuatiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam Mhe. Beatrice Mutungi.
   
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akipanda Mti baada ya kuzinduliwa kwa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam. 
                                          
(picha  na Lydia  Churi )

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni