Jumatatu, 5 Februari 2018

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI WAWILI WATEULE WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Mcheche Masaju (wa kwanza kulia) na aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Gerson Mdemu (wa pili kulia) wakila kiapo cha kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kufuatiwa uteuzi wao wa Februari 01, 2018, Majaji hao Wateule waliapishwa Februari 03, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Gerson Mdemu kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Hafla ya kuapishwa kwa Majaji Wateule wa Mahakama Kuu ilifanyika Februari 03, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam 
Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju akizungumza jambo mara baada ya kuapishwa rasmi na Mhe. Rais kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Februari 03, 2018.
Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Gerson Mdemu akisalimiana na Mhe. Rais mara baada ya kuapishwa, aliyesimama kushoto kwa Mhe. Mdemu ni Jaji Mteule wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju. Aidha; kwa sasa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mteule ni Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Mhe. Paul Joel Ngwembe.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni