Jumatatu, 5 Februari 2018

VIKAO VYA MAHAKAMA YA RUFANI VYAANZA: MBEYA WAZINDUA KWA GWARIDE MAALUM

VIKAO VYA MAHAKAMA YA RUFANI VYAANZA RASMI MBEYA WAZINDUA KWA GWARIDE MAALUM.

Vikao vya Mahakama ya Rufani vimeanza kusikilizwa leo Mahakama Kuu Mbeya, vikao hivyo vitakavyodumu kwa muda wa mwezi mmoja vimezinduliwa kwa gwaride maalum lililofanyika katika Viwanja vya Mahakama Kuu Mbeya ambapo Mwenyekiti wa Jopo hili ni Mhe. Jaji Benard Luanda, Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye amelikagua
Wahe. Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani waliopo katika jopo hilo ni Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika na Mhe. Jaji Bethuel Mmila,  katika vikao hivyo vya mwezi mmoj,  jumla ya Mashauri 27 yatasikilizwa huku Mashauri 19 yakiwa ya Jinai na Mashauri nane (8) yakiwa ya Madai. 
Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Benard Luanda akikagua gwaride maalum katika Viwanja vya Mahakama Kuu-Mbeya kuashiria uzinduzi rasmi wa vikao cha Mahakama ya Rufani vilivyoanza rasmi Februari 05, 2018. 
(Picha na Rajabu Singana, Mahakama Kuu-Mbeya)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni