Ijumaa, 23 Machi 2018

MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI WAFANYA KIKAO CHA TATHMINI YA UTENDAJI WA MWAKA 2017 NA KUWEKA MALENGO YA MWAKA HUU 2018



Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akifungua kikao cha Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, lengo la kikao hicho cha siku moja kimelenga katika kufanya tathmini yaUtendaji kazi wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2017 na kuweka Mkakati na malengo ya mwaka, 2018, kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Benard Luanda.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikao hicho akiendesha kikao cha Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, kushoto ni Jaji namba moja wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jaji Mbarouk S. Mbarouk, kulia ni Mhe. Jaji Benard Luanda.

Sehemu ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya ‘Oceanic’ iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya  Rufani pamoja na Wasaidizi wa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika kikao hicho.


 Waheshimiwa Majaji wakimsikiliza Mhe. Jaji Mkuu wakati akitoa neno la ufunguzi.

Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati akitoa Mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliopo katika kikao cha tathmini na uwekaji wa mpango wa malengo ya utekelezaji kwa mwaka huu. 



Msajili-Mahakama ya Rufani (T) akitoa Mada katika Kikao cha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani (T), katika Mada yake Mhe. Msajili amesema kuwa Mahakama ya Rufani imefanikiwa kushusha kiwango cha mlundikano kutoka asilimia 37 mwaka 2016 hadi asilimia 10 mwishoni mwa Desemba, 2017, vilevile kwa mwaka huu 2018, Mahakama ya Rufani imejipanga Kusikiliza Mashauri na Kuimarisha Masjala.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma (katikati) pamoja na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Wasajili ya Mahakama ya Rufani.


Picha ya pamoja: Mhe. Jaji Mkuu, Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Wasaidizi wa Sheria wa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

(Picha na Mary Gwera)
 
 
 





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni