Jumatatu, 23 Julai 2018

MAHAKAMA YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WAKE KUHUSU MASUALA YA HABARI

Na Lydia Churi-Dodoma
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh leo amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa na kuwataka kuzingatia mafunzo hayo ili waweze kutoa taarifa za Mahakama zilizo sahihi zitakazowezesha kuboresha suala zima la utoaji wa haki kwa wananchi.

Akifungua mafunzo hayo mjini Dodoma, Jaji Awadh amesema Mahakama ya Tanzania kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16-2019/20) inakusudia kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na kuimarisha ushirikano na wadau wake. 

Alisema hatua ya Mahakama kuwapatia Mafunzo watumishi pamoja na wadau wake ni moja ya mikakati ya kurejesha imani yake kwa wananchi na kushirikisha wadau katika shughuli za Mahakama kama ambavyo nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015/16-2019/2020) wa Mahakama ya Tanzania inavyosema.

Alisema nguzo ya kwanza ya Mpango Mkakati huo inahusu Utawala Bora na usimamizi wa Rasilimali ambapo nguzo ya pili inahusu upatikanaji wa Haki kwa wananchi kwa wakati.

Aidha, mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari wa Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama Kuu na Mahakama za Mikoa yanawahusisha Watumishi wa Mahakama wakiwemo Maafisa Habari, Maafisa Utumishi, Maafisa Tawala, Maafisa Tehama pamoja na Wasaidizi wa Kumbukumbu.

Mafunzo hayo pia yanawahusisha Maafisa Habari wa Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama ya Tanzania zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria, Wizara ya katiba na Sheria na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 

Akielezea malengo ya mafunzo hayo, Jaji Awadh alisema yatasaidia kuimarisha utoaji wa habari za mahakama kwa wananchi kwa kuwa Maafisa hao watajengewa uwezo utakaowawezesha kuandika taarifa za mahakama zitakazoongeza uelewa kwa wananchi juu ya maboresho yanayoendelea kufanyika na hatimaye kurejesha imani ya wananchi kwa Mhimili huo.

Jaji Awadh aliyataja malengo mengine ya mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kuwapatia ujuzi washiriki hao hasa katika ukusanyaji, uandaaji na utoaji wa taarifa zinazohusu mahakama ya Tanzania pamoja na kuwajengea uwezo Maafisa hao kuhusu matumizi ya Teknolojia katika utoaji wa habari za Mahakama.

Mafunzo ya siku tano kwa watumishi hao wa Mahakama yameandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Kushoto ni Mshauri Mwelekezi wa Mawasiliano kutoka kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama (Judiciary Delivery Unit- JDU) Dkt. Cosmas Mwaisobwa na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe.
Maafisa Habari, Maafisa Tawala, Maafisa Utumishi, Maafisa Tehama na Wasaidizi wa Kumbukumbu wanahudhuria mafunzo hayo. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria.  

 Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia sehemu ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

  Mtoa Mada kwenye mafunzo hayo ambaye ni Mkufunzi kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Bw. Lameck Samson akielezea umuhimu wa mafunzo hayo kwa washiriki.
   Mtoa Mada kwenye mafunzo hayo ambaye pia ni Mshauri Mwelekezi wa Mawasiliano kutoka kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama (Judiciary Delivery Unit- JDU) Dkt. Cosmas Mwaisobwa akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
 Afisa Tawala kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe, Ezra Kyando akichangia mada wakati wa mafunzo. 
 Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Afisa Tawala kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Moses Mongi akichangia mada wakati wa mafunzo. 
 Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Afisa Tawala kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Sauaeli Urio akielezea jambo wakati wa mafunzo.
  
  Afisa Tehama kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga Bi. Amina Ahmad  akielezea jambo wakati wa mafunzo.
   Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria.  
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Mhe. Mohamed Awadh akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiwa Mafunzo ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa habari za Mahakama walioko kwenye kanda za Mahakama kuu ya Tanzania na kwenye Mahakama za Mikoa yaliyoanza leo mjini Dodoma. 
Mafunzo hayo pia yanahudhuriwa na Maafisa habari kutoka baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wa Mahakama zikiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume na Tume ya Kurekebisha Sheria.  

Maoni 1 :