Jumatatu, 29 Aprili 2019

MASHAURI 31 KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA YA RUFANI-IRINGA


Na Lusako Mwang’onda, Mahakama Kuu – Iringa

Jumla ya mashauri thelathini na moja (31) yanatarajiwa kusikilizwa katika vikao maalum vya Mahakama ya Rufani ‘Court of Appeal session’ vinavyofanyika Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa kuanzia Aprili 29, 2019 hadi Mei, 15 mwaka huu.

Akizungumza katika mahojiano maalum, mapema Aprili 29, 2019 Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Amir Msumi alisema jumla ya mashauri ishirini na mbili (22) kati ya hayo ni mashauri ya muda mrefu na mashauri tisa (9) ni mashauri yenye umri wa kati na mapya.

“Mkakati uliopo ni kuhakikisha hali ya kuzalisha mlundikano hasa kwa mashauri yenye umri mkubwa inadhibitibiwa” alisema Mhe. Msumi huku akiongeza kuwa sambamba na kikao hiki vikao vingine vinafanyika Dar es Salaam na Bukoba.

Naibu Msajili huo aliongeza kuwa kikao hicho ni muendelezo wa utekelezaji wa Mpango Maalumu wa kumaliza mlundikano wa mashauri yenye umri mkubwa mahakamani ‘backlogs’ ambacho pia hushughulikia mashauri yenye umri wa kati na mapya ‘back-stopping’.

Ufunguzi rasmi wa hivyo katika Kanda hiyo ulifanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Iringa na umeongozwa na Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kipenka M. Mussa.

Mbali na Mhe. Jaji Kipenka ambaye ndiye Mwenyekiti wa jopo kikao hicho kitaendeshwa na Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani ambao ni Mhe. Jaji Shaaban Lila, Mhe. Jaji Ferdinand Wambali na Mhe. Jaji Winifrida Korosso.
 Mwenyekiti wa jopo la Majaji wanne wa Mahakama ya Rufani (T) waliopo katika kikao cha Mahakama hiyo mkoani Iringa, Mhe. Jaji Kipenka Mussa (mwenye joho jekundu) akikagua gwaride maalum kuashiria ufunguzi rasmi ya kikao cha Mahakama ya Rufani kitakachofanyika Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kuanzia Aprili 29, 2019 hadi Mei 15, 2019.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni