Alhamisi, 19 Septemba 2019

WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAPIMA HOMA YA INI


Na Aziza Muhali. (SJMC)

Daktari Bingwa wa Virusi vinavyosababisha Saratani ambaye pia ni mtafiti anayefanya tafiti za seli za saratani kutoka Taasisi ya Saratani ‘Ocean Road’, jijini Dar es Salaam, Kandali Samweli, amewataka watumishi wa Mahakama ya Tanzania kujitokeza
 mapema kuchunguza afya zao na kupata chanjo dhidi ya maambukizi ya homa ya Ini ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo. 

Wito huo umetolewa, leo Septemba 19, 2019 na Daktari huyo wakati wa utoaji elimu, upimaji hiari na utoaji chanjo dhidi ya homa ya Ini kwa watumishi hao, kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, unaoendelea kufanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Mahakama Kuu, uliopo jijini Dar es Salaam, ambapo takribani watumishi 170 wanatarajiwa kufanyiwa kipimo cha ugonjwa huo kwa hiari.

Akizungumza na watumishi hao, mahakamani hapo, Dkt, Samweli, amesema chanjo hiyo hutolewa kwa awamu tatu, ambapo ya kwanza hutolewa mara baada ya kipimo cha Hepatitis B, ya pili hutolewa mwezi mmoja baada ya chanjo ya kwanza, na chanjo ya tatu hutolewa miezi sita baada ya chanjo ya kwanza.  

Dkt. huyo alieleza kuwa katika makundi ya virusi vya ‘Hepatitis’ A, B, C na D homa ya ini husababishwa na kirusi aina ya ‘Hepatitis B’. Hivyo tafiti zinaonyesha kwamba mtu mmoja kati ya ishirini anamaambukizi ya ‘Hepatitis B’.

 Alifanunua  kuwa chanjo hiyo ilianza kutolewa kwa watoto mnamo mwaka 2002 ambapo chanjo hiyo huambatanishwa na chanjo nyingine zinazotolewa punde mtoto anapozaliwa.

‘Chanjo hii ilianza kutolewa mwaka 2002 kwa watoto na inaambatanishwa na chanjo nyingine kwenye kadi ya mtoto, hivyo wanaotakiwa kupata chanjo hii ni waliozaliwa mwaka 2001 na miaka ya nyuma, na tayari tumeshaanza kutoa chanjo hii kwa watu wengine.’ alisema Dkt. Samweli.

Alisema chanjo hiyo hutolewa kwa rika na jinsia zote, na ni salama kwa wajawazito na wanawake wanaonyonyesha.  

Alizungumzia kuhusu dalili za ugonjwa  huo, alisema  hazionekani kwa urahisi kwani hujitokeza baada ya muathirika kuathirika kwa muda mrefu.

 Alizitaja baadhi ya njia zinazoweza kusababisha maambukizi  ya ugonjwa huo, kuwa ni  kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua, mgusano baina ya mtu na mtu kupitia damu na majimaji mengine ya mwili, ngono zembe, kuchangia vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye virusi hivyo  na kuongezewa damu iliyoathiriwa na virusi hivyo.

Aidha  jamii inatakiwa kuchunguza afya zao kwa kupata kipimo hicho, ikiwemo   chanjo mapema kwani mtu anaweza kupata virusi hivyo bila dalili kujitokeza, kwani dalili zinajitokeza baada ya madhara makubwa,’ alisisitiza huku akisema  athari za kuishi na virusi vya Hepatitis B pasipo tiba huweza kusababisha Saratani ya Ini.

Kwa upande wake Naibu Msajili Mahakama Kuu, Mhe. Devotha Kamuzora, amesema kuwa huduma hiyo ya utoaji chanjo dhidi ya homa ya ini ni nzuri na imerahisishwa kwa kuletwa karibu yao kwani imewasaidia watumishi kujua hali zao juu ya  ugonjwa huo, pia kuchukua tahadahari dhidi ya maambukizi.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) akipatiwa elimu kuhusu upimaji wa ugonjwa wa homa ya ini leo na Daktari Bingwa vya Virusi vya  Saratani, Kandali Samweli (wa pili kulia) kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam wakati wa kampeni ya upimaji wa hiari wa ugonjwa huo unaofanyika kwa Watumishi wa Mahakama Kuu na  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo  unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam.



Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Gaston Kanyairita  (kulia) akimsikiliza Daktari Bingwa vya Virus vya Saratani, Kandali Samweli (wa pili kulia) kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam  wakati akitoa elimu  wa upimaji wa hiari wa homa ya ini  unaofanyika kwa Watumishi wa Mahakama Kuu  na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, (katikati) ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Peter Machalo, (aliyesimama)ni Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Wilbert Chuma.


Daktari Bingwa vya Virusi vya  Saratani, Kandali Samweli (katikati) kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam, amkipatia elimu kuhusu upimaji wa homa ya ini Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.Leila  Mgonya, (wa pili kulia)n wakati wa uhamasishaji wa upimaji wa hiari wa ugonjwa huo  unaofanyika kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu.Kulia wa kwanza ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Lucy Tungaraza na kushoto wa kwanza Muuguzi, Bi. Odilia Masawe na Mtaalam wa Maabara, Bw. Costantine Anga wote wanatoka katika taasisi hiyo.

Daktari Bingwa  vya Virusi vya  Saratani, Kandali Samweli ( wa pili kushoto ) kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam, amkipatia elimu kuhusu upimaji wa homa ya ini Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Joseph Mlyambina wakati wa uhamasishaji wa upimaji wa hiari wa ugonjwa huo  unaofanyika kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu.  




Daktari Bingwa vya Virusi vya Saratani, Kandali Samweli, kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam akiwapatia elimu  kuhusu  upimaji wa ugonjwa  wa homa ya ini  Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu, wakati wa upimaji huo unaoendelea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam. 

Daktari Bingwa vya Virusi vya Saratani, Kandali Samweli kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam akionyesha kadi ambayo mtu hupatiwa baada ya kupata chanjo   ugonjwa wa homa ya ini  kwa Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu, alipokuwa akitoa elimu kuhusu upimaji huo.

Afisa TEHAMA wa Mahakama Kuu, Bi. Mwanaisha Mkweya akifanyiwa kipimo cha ugonjwa wa homa ya ini na Mtaalamu wa Maabara kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Bw. Constantine Anga.

Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama Kuu, Bw. Kenedy Nsenga akifanyiwa kipimo cha ugonjwa wa homa ya ini na Mtaalamu wa Maabara kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Bw. Constantine Anga.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu wakiwa katika foleni kwa ajili ya kuweza kufanyiwa vipimo vya ugonjwa wa homa ya ini unaoendelea kufanyika katika ukumbi Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mahakama Kuu wakiwa katika foleni kwa ajili ya kuweza kufanyiwa vipimo vya ugonjwa wa homa ya ini unaoendelea kufanyika katika ukumbi Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.


Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Devotha Kamuzora (wa pili kushoto) akijiandikisha kwa ajili ya upimaji wa ugonjwa wa homa ya ini. Kushoto wa kwanza ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Nyigulila Mwasoba. Kulia ni Mfamasia kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, iliyopo jijini Dar es Salaam, Bw. Joseph Ryoba.

(Picha na Magreth Kinabo)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni