Alhamisi, 15 Oktoba 2020

MIRADI YA UJENZI WA MAHAKAMA YASHIKA KASI JIJINI DODOMA

Na Stanslaus Makendi, Mahakama Kuu Dodoma

Mahakama ya Tanzania inatekeleza miradi mbalimbali ya ukarabati na ujenzi wa Mahakama nchini kwa lengo la kuboresha miundombinu yake ili kuwa na mazingira wezeshi ya utaoji wa huduma ya utoaji haki kwa ujumla.

Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa kadhaa nchini ambapo miradi mikubwa ya ujenzi wa Mahakama inaendelea. Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Mahakama ya Tanzania inatekeleza jumla ya miradi mitano ya ujenzi wa Mahakama katika Mkoa huo; ikiwemo ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama, Kituo Jumuishi ya Utoaji haki (Intergrated Justice Centre), Mahakama za Wilaya Chemba na Bahi na Mahakama ya Mwanzo Kibaigwa.

Aidha, hatua ya maboresho ya miundombinu ya majengo ya Mahakama nchini inalenga pia kusogeza huduma za haki karibu zaidi na wananchi ili kumuwezesha mwananchi kupata huduma kwa haraka kwa kupunguza umbali na gharama katika kutafuta huduma ya haki.

Pichani ni miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea jijini Dodoma.


Shughuli za ujenzi zikiendelea kwa kasi katika eneo la mradi wa ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama 'NCC Link' - Dodoma. 
Hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa kituo jumuishi cha utoaji haki Dodoma (Intergrated Justice Centre). Mkandarasi Hainan International Ltd.
Mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Bahi ukiwa katika hatua za mwisho wa utekelezwaji wake. Mkandarasi Moladi Tanzania Ltd.

Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya Chemba ukiendelea; ikiwa ni hatua muhimu katika uanzishaji wa huduma za Mahakama katika Wilaya ambazo hazikuwa na Mahakama hapo awali. Mkandarasi wa mradi huu wa ujenzi ni 'Moladi Tanzania Ltd.'
Ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kibaigwa ukiendelea kwa lengo la kusogeza huduma za Haki karibu na wakazi wa eneo hilo, awali walilazimika kupata huduma hiyo nje kabisa ya Mji wa Kibaigwa. Mkandarasi Moladi Tanzania Ltd.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni