Jumatatu, 21 Desemba 2020

IJA YATOA TUZO KWA VIONGOZI WA MAHAKAMA KWA MCHANGO WAO

Na Lydia Churi-Mahakama

Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kimetoa tuzo kwa Viongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kutambua na kuthamini mchango wao katika kukiwezesha chuo hicho kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kuisadia Mahakama.

Tuzo hizo zimetolewa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi wakati wa Mahafali ya Ishirini ya Chuo hicho pamoja na kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka ishirini ya chuo hicho, yaliyofanyika Desemba 18, 2020 wilayani Lushoto.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akipokea Tuzo iliyotolewa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kutambua mchango wake katika maendeleo ya chuo hicho. Anayemkabithi Tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Gerald Ndika wakati wa Mahafali ya Ishirini ya Chuo hicho Desemba 18, 2020. 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akionesha Tuzo hiyo. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akipokea Tuzo iliyotolewa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kutambua mchango wake katika maendeleo ya chuo hicho. Anayemkabidhi Tuzo hiyo ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Paul Kihwelo. Jaji Kiongozi amekabidhiwa Tuzo ofisini kwake kwa kuwa hakuweza kuhudhuria Mahafali yaliyofanyika Lushoto.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akionesha Tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni