Jumatano, 27 Januari 2021

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA MAONESHO YA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Mahakama pindi alipotembelea banda la miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania mapema Januari 27, 2021. Maonesho ya Wiki ya Sheria kwa mwaka huu yanaenda sambasamba na maadhimisho ya miaka 100 ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Maonesho kama haya yanafanyika nchi nzima


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi akiangalia orodha ya Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu ya Tanzania waliopo kazini na waliostaafu.


Prof. Kilangi akipata maelezo kutoka katika banda la Kurugenzi la Uendeshaji mashauri.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipata fursa pia ya kutembelea banda la Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Mhe. Prof. Kilangi akiwa katika banda la Malalamiko.

Akiwa katika banda la Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ).

Magereza

Akipata ufafanuzi wa masuala kadhaa kutoka Maafisa wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya.

(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni