Jumapili, 14 Februari 2021

MTUMISHI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA BUKOMBE AFARIKI DUNIA

                                 TANZIA 


Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukombe, Minza Shiyi aliyekuwa Karani wa Mahakama ya Mwanzo Runzewe kilichotokea jana jioni ,Februari 13, 2021.

Mahakama ya Tanzania inatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni