Alhamisi, 15 Aprili 2021

KUNDI LA PILI LA NAIBU WASAJILI NA WATENDAJI WAANZA MAFUNZO YA UTUNZAJI KUMBUKUMBU

Matukio katika picha, hafla fupi ya ufunguzi rasmi wa Mafunzo elekezi ya Utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka za Mahakama kwa kundi la pili la Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi aliyefungua Mafunzo hayo amewasisitiza Washiriki hao kuendelea kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuboresha huduma za Mahakama kwa manufaa ya wananchi.

Katika mafunzo hayo ya siku tatu (3) yaliyoanza rasmi leo Aprili 15, 2021 hadi Aprili 17, 2021 Washiriki watapitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya majalada na uandishi wa nyaraka mbalimbali, usajili wa mashauri kwa mfumo wa kielektroniki, usimamizi na ukaguzi wa Mahakama, usimamizi wa masuala ya fedha na kumbukumbu zake kupitia mfumo mpya wa ‘MUSE’ na mifumo ya ndani na usimamizi wa bajeti.

Baadhi ya Naibu Wasajili na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wanaoshiriki katika Mafunzo elekezi ya siku tatu (3) ya Utunzaji bora wa kumbukumbu na Nyaraka wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Mafunzo hayo yanayotolewa kwa kundi la pili la Maafisa hao yamefunguliwa rasmi leo Aprili 15, 2021 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango kilichopo jijini Dodoma.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Mustapher Siyani akifungua rasmi Mafunzo ya siku tatu (3) ya Utunzaji bora wa kumbukumbu na Nyaraka kwa kundi la pili la Wasajili na Watendaji wa Mahakama. Mafunzo hayo yanayotolewa kwa kundi hilo yamefunguliwa rasmi leo Aprili 15, 2021 na yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango kilichopo jijini Dodoma.


Picha mbalimbali za Wahe.Wasajili na Watendaji wa Mahakama wanaoshiriki katika Mafunzo hayo.

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha akizungumza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mafunzo hayo.


Mgeni rasmi ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe. Mustapher Siyani (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Waheshimiwa Naibu Wasajili wanaoshiriki katika Mafunzo hayo. Aliyeketi kushoto ni Mhe. Kevin Mhina, Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na kulia ni Bw. Leonard Magacha, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.


Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wasajili wanaoshiriki katika mafunzo hayo.

(Picha na Mary Gwera, Mahakama)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni