Alhamisi, 30 Juni 2022

MAHAKAMA YA TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA SABASABA 2022

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 

MAHAKAMA YA TANZANIA

  

TANGAZO KWA UMMA

MAHAKAMA YA TANZANIA INAPENDA KUWAJULISHA WANANCHI NA WADAU WOTE KWA UJUMLA KUWA INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 46 YA BIASHARA YA KIMATAIFA ‘SABASABA’ KUANZIA TAREHE 28 JUNI, 2022. KATIKA KIPINDI CHA MAONESHO HAYO, MAHAKAMA ITAKUWA IKITOA HUDUMA ZIFUATAZO: -

1. HUDUMA YA KUSIKILIZA MASHAURI MAHAKAMA INAYOTEMBEA ‘MOBILE COURT SERVICES’

2. KUTOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI YA TEHAMA MAHAKAMANI NA SAFARI YA MAHAKAMA KUELEKEA MAHAKAMA MTANDAO ‘e-JUDICIARY’.

3. ELIMU KUHUSU HUDUMA NA TARATIBU MBALIMBALI ZA UFUNGUAJI WA MASHAURI YAKIWEMO MASHAURI YA MIRATHI.

4. KUELEZEA MFUMO WA KUSAJILI, KURATIBU NA KUSIMAMIA UENDESHAJI WA MASHAURI (JSDS II)

5.KUTOA MAELEKEZO YA UPATIKANAJI WA UAMUZI KWA NJIA YA MTANDAO

6. KUELEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA NGAZI MBALIMBALI ZA MAHAKAMA IKIWEMO DIVISHENI ZA MAHAKAMA KUU

7. KUSIKILIZA NA KUTOLEA SULUHU MALALAMIKO YA WANANCHI

8. KUTOA FOMU ZA UDAHILI NA KUZIPOKEA AMBAPO HUDUMA HII ITATOLEWA NA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA)

9. MSAADA WA KISHERIA ‘TLS’

10. KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUTAMBUA UMUHIMU WA KUTUMIA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA ‘CALL CENTRE’ YA MAHAKAMA YA TANZANIA KUTOA MALALAMIKO NA MAONI YAO.

AIDHA; KATIKA MAONESHO HAYO MAHAKAMA YA TANZANIA IPO KATIKA BANDA MOJA PAMOJA NA BAADHI YA WADAU WAKE AMBAO NI CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA-LUSHOTO, (IJA), TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA (JSC), CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA), CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS), PAMOJA NA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI (EACJ), AMBAO WOTE WATATOA ELIMU KUHUSU MAENEO YAO.

HUDUMA TAJWA ZINATOLEWA NDANI YA BANDA LA MAHAKAMA, LILILOPO MKABALA NA BANDA LA JKT KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE ‘SABASABA’ JIJINI `DAR ES SALAAM.

HUDUMA HIZO ZITATOLEWA KUANZIA TAREHE 28 JUNI HADI HADI JULAI 08, 2022.

EWE MWANANCHI, KARIBU UPATE ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.

WOTE MNAKARIBISHWA.

IMETOLEWA NA; 

KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,

 MAHAKAMA YA TANZANIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni