Jumapili, 24 Machi 2024

JAJI MFAWIDHI MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM AFUTURISHA WATUMISHI

Na Eunice Lugiana, Mahakama-Dar es Salaam

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi amekutana na watumishi wa Kanda hiyo kwa ajili ya kupata ‘Iftar’ pamoja nao katika mfungo mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati wa Iftar hiyo tarehe 22 Machi, 2024 iliyofanyika Mahakama Kuu-Dar es Salaam, Mhe. Maghimbi alisema funga mbili zimekutana kwa pamoja yaani funga ya Kwaresma na funga ya Ramadhani hivyo ameona ni vema kukutana  kama Waislamu na Wakristo wakae kwa pamoja  kama timu.

“Lengo la kukutana  ni kukaa pamoja ili tuongee, tufurahi, tupendane na  kuzoeana kisha tuendelee kuchapa kazi, lakini nawaomba sana baada ya leo tuendela kupendana tuwe na umoja tukisema kuna shughuli tuitikie sio tena tuanze kunyata,” alisema Jaji Mfawidhi.

Aidha akitoa salaam za shukrani, Mhe. Maghimbi alisema kwa sababu kazi zinakwenda hawana budi kukaa pamoja na kufurahi kwa pamoja akiahidi kuwa, wakati mwingine wataenda kwenye shughuli nyingine ambayo itawafanya kuwa pamoja na kufurahi.

Naye, Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Sundi Fimbo alimshukuru Mhe. Maghimbi na kukiri kwamba, kitendo hicho kimewaonesha ukarimu na upendo wa dhati.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Masjala Kuu wakipata Iftar iliyoandaliwa na Jaji Mfawidhi  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi.
Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Masjala Kuu wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe.Aziza Mbadjo (wa tatu kulia waliosimama mbele).
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi akitoa neno kabla ya kupata Iftar na Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salama na Masjala Kuu.
Majaji Wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  wakiongozwa na Jaji Mfawidhi, Mhe. Salma Maghimbi (wa tatu kushoto). Kutoka Kulia ni Mhe. Elizabeth Mkwizu, Mhe. Hamidu Mwanga, Mhe. Awamu Magwa, Mhe. David Ngunyale na Mhe. Anorld Kirekiano.
 

Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Sundi Fimbo akitoa neno la shukrani kwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Mhe. Maghimbi.

Naibu Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mshereheshaji katika Iftar hiyo, Mhe. Aziza Mbadjo akizungumza jambo.

(Habari hii imehaririwa na Mary Gwera, Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni