Alhamisi, 21 Machi 2024

WAJUMBE BARAZA LA ELIMU YA SHERIA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA MAHAKAMA TANZANIA

Na Brian Haule, Mahakama Makao Makuu, Dodoma

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria juzi tarehe 19 Machi,2024 walipata nafasi ya kutembelea Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania mara baada ya kumaliza kikao cha siku mbili cha kwanza kwa mwaka 2024.

Kikao hicho cha siku mbili kilichoongozwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyaniambaye ndio Mwenyekiti wa Baraza hilo kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo Jumuishi Dodoma kuanzia tarehe 18 Machi, 2024.

Wajumbe hao ni Bi. Frida Mwela kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Erasmo Nyika kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mutabaazi Lugaziya kutoka Ofisi ya Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Bw. Silwan Mwantembe kutoka Ofisi ya TLS.

Wajumbe hao waliongozana na Katibu wa Baraza la Elimu ya Sheria, ambaye pia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Elimo Massawe.

Wakiwa katika jengo hilo jipya la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania lililopo katika eneo la Tambukaleli Dodoma, wajumbe hao walitembelea ofisi mbalimbali, ikiwemo Ofisi ya Jaji Mkuu, Ofisi ya Jaji Kiongozi, Ofisi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Ofisi ya Kitengo cha Utoaji wa Huduma kwa Wateja.

Walionesha kufurahishwa na maboresho yanayoendelea kufanyika Mahakamani na kupongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kufanikisha Maboresho hayo.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria (wa pili kutoka kulia ni Mhe. Silwan Galati, wa katikati ni Mhe. Elimo Massawe, na wa tatu kutoka kulia ni Mhe. Frida Mwela) wakimsikiliza Bw. Witness Ndenza aliyesimama mbele yao, ambaye ni Afisa TEHAMA akiwaeleza kuhusu Huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama kupitia TEHAMA.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria, wa pili kutoka kulia Mhe. Elimo Massawe, wa tatu kutoka kulia Mhe. Frida Peter Mwela, wa nne kutoka kulia Mhe. Silwan Mwantembe Galati, wa tano kutoka Kulia ni Mhe. Dkt. Mutabaazi Lugaziya, na aliyesimama kushoto ni Mhe. Dkt. Erasmo Nyika wakimsikiliza Bw. Witness Ndeza (AFISA TEHAMA) aliyekuwa akiwapatia maelezo kuhusu masuala ya TEHAMA.

Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria (CLE), wa kwanza kushoto ni Mhe. Elimo Massawe (Katibu wa Baraza), wa pili kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Mutabaazi Lugaziya, wa tatu kutoka kushoto ni Mhe. Frida Peter Mwela, wa nne kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Erasmo Nyika na wa tano kutoka kushoto ni Mhe. Silwan Mwantembe Galati, wakiwa katika picha ya pamoja katika Jengo jipya la Mahakama ya Tanzania Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria (CLE), wakikagua mojawapo ya Ofisi zilizopo katika Jengo hilo (Call Center) wakiwa pamoja na Maafisa TEHAMA Bw. Witness Ndenza na Bw. Juma Kimaro. ambao hawajavaa makoti ya Suti.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni