Jumatatu, 25 Machi 2024

WAJUMBE WA MENEJIMENTI MAHAKAMA SONGEA WAKUTANA

Na Hasani Haufi- Mahakama Songea

Menejimenti ya Mahakama, Kanda ya Songea, hivi karibuni ilifanya kikao kutathmini utendaji kazi katika kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Kikao hicho kilichofanyika wilayani Songea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chandamali kilifunguliwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti katika kikao hicho.

Mhe. Karayemaha aliwataka wajumbe wa kikao hicho kuzingatia maelekezo ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Viongozi wa ngazi za juu kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika huduma za utoaji haki.

Wakati wa kikao hicho, kulikuwa na taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mahakama kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2024, ambayo iliwasilishwa na Katibu ambaye ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Bw. Epaphras Tenganamba.

Katika taarifa yake, Bw. Tenganamba alieleza masuala mbalimbali, ikiwemo utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali.

Kwa upande wake, Afisa Bajeti wa Mahakama Kanda ya Songea, Bi. Paulina Kapinga aliwasilisha maoteo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na maombi ya fedha ya nyongeza.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha (katikati) akizungumza na wajumbe wa kikao cha menejimenti Mahakama Kanda ya Songea. Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele na kula ni Mtendaji wa Mahakama, Kanda ya Songea, Bw. Epaphras Tenganamba.

Sehemu ya wajumbe (juu na chini) wakimfuatilia kwa karibu Mwenyekiti wa kikao (hayupo kwenye picha).

Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Bw. Epaphras Tenganamba, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mahakama.

Afisa Bajeti Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Bi. Paulina Kapinga, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji bajeti ya robo ya tatu ya mwaka 2023/2024.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni