Jumatatu, 6 Mei 2024

KITUO JUMUISHI TEMEKE CHAJIPANGA UENDESHAJI MASHAURI YA NDOA, TALAKA

Na Mary Gwera, Mahakama-Dar es Salaam

Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia na Mirathi-Temeke kimefanya Mafunzo ya kubadilishana uzoefu kuhusiana na mashauri ya ndoa na talaka ili kujenga uelewa wa pamoja kwenye mienendo na maamuzi ya mashauri yanayoendeshwa katika Mahakama hiyo.

Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Jaji Mfawidhi Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa aliwapongeza washiriki wote kuweza kushiriki na kueleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwa na uelewa wa pamoja katika mambo ya msingi ya kuzingatia katika maamuzi ya mashauri ya ndoa kwa kuzingatia msingi wa sheria na taratibu husika.

“Mafunzo haya ni mpango wa uongozi wa Kituo yaani utawala wa kituo, ambapo Sekretarieti ya mafunzo hupokea maoni kutoka Majaji na Mahakimu kuhusu maeneo yenye utata na mkanganyiko ili kujenga uelewa wa pamoja kwenye mienendo na maamuzi,” alisema Jaji Mfawidhi Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa.

Mhe. Mnyukwa aliongeza kuwa, Mafunzo hayo hulenga kujenga uelewa wa pamoja katika uamuzi wa mashauri ya ndoa na talaka kwa mujibu wa Sheria pamoja na kupeana mbinu za utambuzi na uamuzi ili kuendana na mazingira husika ya mashauri ya ndoa.

Akitoa Mada kuhusu muongozo wa Sheria katika vipengele muhimu ambavyo Mahakimu walipendekeza kuhitaji kupata ufafanuzi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Elizabeth Mkwizu aliwasilisha kwa kugusa vipengele muhimu ambavyo ni pamoja na Mambo ya msingi ya kuzingatia wakati wa kuamua mgawanyo wa machumo kisheria, Taratibu zinazopaswa kufuatwa katika kujaza fomu za kushindikana kwa usuluhishi wa mashauri ya ndoa kutoka katika Mabaraza ya usuluhishi wa mashauri ya ndoa.

Vipengele vingine alivyofafanua Mhe. Mkwizu ni juu ya Mamlaka ya kisheria kuhusu mashauri ya dhana ya ndoa kwa Mahakama za Mwanzo, ⁠Nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa mahakamani wakati wa kufungua mashauri ya ndoa na dhana ya ndoa.

Kadhalika, Jaji Mkwizu alizungumzia kuhusu ⁠Uhalali wa kutoa hati ya talaka kwenye dhana ya ndoa kisheria, upokeaji wa ushahidi wa kielektroniki katika Mahakama za Mwanzo.

Baada ya Wasilisho, washiriki walipata nafasi ya majadiliano na kuazimia kuwa, Mgawanyo wa machumo uzingatie msingi wa Sheria kwa kuzingatia Mchango wa Wanandoa katika upatikanaji wa mali husika na kanuni ya usawa (fairness), Mabaraza ya Usuluhishi yanapaswa kueleza maoni yake kwenye fomu namba 3 kwa uwazi kuhusu kushindikana kwa usuluhishi.

Maazimio mengine yaliyofikiwa katika Mafunzo hayo ni kwamba, Mahakama ya mwanzo ina mamlaka ya kushughulikia mashauri ya dhana ya ndoa kwa mujibu wa Sheria kama Mahakama zingine kwakuwa Mahakama ya Mwanzo, Wilaya na Kuu zina mamlaka sawa kuhusu mashauri ya ndoa na talaka.

Mengine ni Mahakama ya Mwanzo ijikite kutumia Kanuni za Ushahidi katika Mahakama za Mwanzo katika kupokea ushahidi na sio Sheria ya Ushahidi hasa kwenye ushahidi wa kielektroniki na kadhalika.

Akifunga Mafunzo hayo, Jaji wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke, Mhe. Gladys Barthy alimshukuru Jaji Mfawidhi kwa kuandaa mafunzo hayo na vilevile alimshukuru Jaji Mkwizu kwa uwasilishaji mzuri na kuwashukuru washiriki wote kushiriki katika Mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 03 Mei, 2024 katika Kituo hicho kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam ni moja ya mfululizo wa mafunzo ya ndani ya Kituo hicho kwa ajili ya Majaji na Mahakimu wanaohudumu katika Kituo hicho ambayo hufanyika kila baada ya miezi mitatu (3).

Sehemu ya Watumishi wa Mahakama wakiwemo Naibu Wasajili na Mahakimu wanaohudumu katika Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke wakiwa katika Mafunzo ya kubadilishana uzoefu kuhusiana na mashauri ya ndoa na talaka yaliyofanyika Kituoni hapo mwishoni mwa Wiki iliyopita.
Jaji Mfawidhi Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (kulia) akiwa katika Mafunzo ya kubadilishana uzoefu kuhusiana na mashauri ya ndoa na talaka yaliyofanyika hivi karibuni. Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Elizabeth Mkwizu akitoa mada.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Elizabeth Mkwizu (kushoto) akitoa mada. Wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa, wa pili kulia ni Jaji Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Gladys Barthy na kulia ni Jaji wa Kituo hicho, Mhe. Asina Omari.

(Picha na Mary Gwera, Mahakama)




 

Maoni 1 :

  1. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta