Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia-Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa jana 09 Julai, 2024 alipata wasaa wa kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), 2024 yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Temeke jijini Dar es Salaam.
Jaji Mnyukwa aliwasili katika banda la Mahakama majira ya saa 9 alasiri ambapo alipata fiursa ya kutembelea mabanda ya Mahakama pamoja na ya Wadau yaliyomo ndani ya Banda la Mahakama ya Tanzania.
Mabanda aliyotembelea ni Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri, Idara ya Kumbukumbu na Maktaba, Mahakama Kuu Kituo cha Usuluhishi, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mahakama Kuu Divisheni Kazi, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Kurugenzi ya Malalamiko, Ukaguzi wa Huduma za Mahakama na Maadili, Kituo cha Huduma kwa Mteja, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mabanda mengi yote yaliyomo ndani ya banda la Mahakama.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za ziara yake;
Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa akipata maelezo kutoka kwa Mtumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi.
Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa akizungumza na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Watoto Temeke, Mhe. Orupa Mtae (kulia).
Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Mahakama ya Tanzania, Mhe. Denice Mlashani akitoa maelezo kwa Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke wakati alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya Sabasaba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni