Alhamisi, 15 Agosti 2024

UJUMBE KUTOKA OFISI YA MASHTAKA ZANZIBAR NA BARA, WATEMBELEA MAHAKAMA

Na JEREMIA LUBANGO – Mahakama, Dodoma

 

Ujumbe kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bara, Bibiana Kileo pamoja na timu nzima ya kitengo cha TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bara, wametembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma jana tarehe 14 Agosti, 2024 kwa ajili ya kujifunza na kuipongeza Mahakama kwa hatua kubwa iliyopiga kwa upande wa miundombinu ya TEHAMA.

 

Katika wasilisho lake, Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA, Bw. Allan Machela amesema Mahakama ya Tanzania imeweka jitihada nyingi sana kuboresha mifumo yake ikiwa na Pamoja na kwenda kujifunza mifumo ya TEHAMA kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kupata ujuzi na maarifa ya namuna mifumo inavyoweweza kutusaidia.

 

“Hivi vitu sisi tunakuwa na wazo tu, lakini nilazima pia tungalie na wenzetu kwingie wamefanyaje, tukiangalia kwetu kipo lakini kule hakipo tulifanya ‘benchmarking’ kwa nchi zaidi ya tatu ikiwemo kazakhastan na Lithuania ndipo tukaja na mfumo wetu ambao utasaidia kutatua changamoto zetu” Alisema.

 

Baada ya hapo ujumbe kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar na Bara na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bara na Maafisa mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA Bw. Machela walitembelea Chumba cha Mifumo ya kutolea taarifa Muhimu za Mahakama (Judiciary Situation Room).

 

Wakiwa kwenye chumba hicho, walipata maelezo kutoka kwa Maafisa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania na kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa hatua kubwa waliyopiga katika miundombinu ya TEHAMA na wakaomba kuja siku nyingine ili waweze kujifunza Zaidi.

 

Naye, Naibu Mkurugenzi Zanzibar ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa hatua kubwa waliyopiga katika uendeshaji wa mifumo ya TEHAMA kwani kupitia mafunzo hayo wamepata elimu kubwa itakayowasaidia katika utendaji kazi wao.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA Bw, Allan Machela kutoka Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kwa niaba ya timu nzima ya TEHAMA wameushukuru ujmbe kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa ujio wao kutembela Mahakama Pamoja na kujionea namna mifumo ya TEHAMA inavyofanya kazi kwani ni njia mojawapo ya kuendelea kufahamiana na kukuza ushirikiano baina taasisi hizi na Mhimili wa Mahakama.


Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA, Bw. Allan Machela (aliyesimama) akiwasilisha mada kwa Ujumbe kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar na Bara Pamoja na timu nzima ya kitengo cha TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  walipo tembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma jana tarehe 14 Agosti, 2024.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bara Bibiana Kileo akichangia mada kwa ujumbe huo, walipo tembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma jana tarehe 14. Agosti, 2024.


Afisa TEHAMA kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. Lazaro Sanga aliye simama (Kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa Ujumbe huo mara tu walipo tembelea Chumba cha Mifumo ya kutolea taarifa Muhimu za Mahakama (Judiciary Situation Room).


Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Bi. Mwanamkaa Mohammed (mwenye ushungi mweupe) na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bara Bi. Bibiana Kileo (mwenye koti jekundu) wakiwa katika picha ya Pamoja na Watumishi wa Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Ofisi ya Mashtaka Bara, na Maafisa kutoka Mahakama ya Tanzania jana tarehe 14 Agosti, 2024.



Afisa TEHAMA kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. Samweli Mshote aliyesimama (Kushoto) akitoa maelezo mafupi juu ya mfumo (CMS )kwa Ujumbe huo mara tu walipo tembelea Chumba cha Mifumo ya kutolea taarifa Muhimu za Mahakama (Judiciary Situation Room)

  

  

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni