Alhamisi, 19 Septemba 2024

HAKIMU MKAZI MFAWIDHI MPYA KIGOMA ARIPOTI KATIKA KITUO CHAKE

Akoshwa na mapokezi makubwa ya Watumishi wa Mahakama hiyo

Aushukuru uongozi kwa uteuzi kushika nafasi hiyo

Na AIDAN ROBERT, Mahakama-Kigoma

Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigoma, Mhe. Eva Balthazar Mushi, ameongoza watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma kumpokea Hakimu Mkazi Mfawidhi mpya wa Mahakama hiyo, Mhe. Aristida Tarimo alipowasili katika viunga vya Mahakama hiyo tarehe 17 Septemba, 2024. 

Akimkaribisha Mfawidhi huyo wa Mkoa, Mhe. Mushi alisema Kituo kipo salama na amemjulisha kuwa Mahakama hiyo ina wafanyakazi wenye uadilifu, weledi na uwajibikaji katika kazi zao. Aidha, ameongeza kuwa Kituo cha Kigoma ni sehemu nzuri ya kufanya kazi kutokana na mazingira yake kuwa mazuri.

Akizungumza na watumishi hao mara baada ya mapokezi hayo, Mhe. Tarimo  alisema, “hakika Kigoma mnafanya tofauti kwa mapokezi haya ni dalili kuwa tutafanya kazi vizuri na kwa upendo mkubwa hakika najivunia kuwa na watumishi wenye furaha na hamasa kubwa kama hii.”

 Aidha, Hakimu Mkazi Mfawidhi huyo aliwashukuru pia watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma kwa mapokezi mazuri ambayo yamempa mshangao mkubwa kwa upendo waliokuwa nao. 

“Naushukuru Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kuona kuwa mimi naweza kuziba pengo la Mhe. Rose Kangwa aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma aliyeteuliwa kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, nimeona na nimeambiwa mafanikio ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma na sifa ya Kigoma ni uadilifu, weledi na uwajibikaji na matumizi mazuri ya mfumo hivyo tuendelee kama sifa,” alisema, Mhe. Tarimo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kigoma,  Mhe. Aristida Tarimo akipokea maelezo ya awali kutoka kwa Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigoma, Mhe Eva Mushi (hayupo katika picha) wakati Mhe. Tarimo aliporipoti katika Kituo chake cha kazi tarehe 17 Septemba, 2024.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kigoma,  Mhe. Aristida Tarimo (kushoto) akipokelewa na kukabidhiwa zawadi ya ua kutoka kwa Msaidizi wa Kumbukumbu, Bi. Christina Mpungu ikiwa ni ishara ya upendo na furaha ya ujio wake katika Kituo chake cha kazi kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kigoma,  Mhe. Aristida Tarimo akisalimiana  na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kigoma, Mhe. Gadiel Mariki wakati alipowasili katika Kituo chake cha kazi . 

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kigoma,  Mhe. Aristida Tarimo (kushoto) akisalimiana  na Msaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, Bw. Ramadhani Kufakunoga. 

 

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kigoma, Mhe. Aristida Tarimo akisalimiana  na  Afisa Tawala wa Mahakama hiyo, Bw. Ally Khatibu. 

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kigoma,  Mhe. Aristida Tarimo (wa pili kushoto), kushoto kwa Mhe. Tarimo ni Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigoma,  Mhe. Eva Balthazar Mushi akifuatiwa na Msaidizi wa Kumbukumbu Bi. Christina Mpungu, wa kwanza kushoto ni Afisa Tawala wa Mahakama hiyo, Bw. Ally Khatibu na waliosimama nyuma ni watumishi wa Mahakama hiyo.  

(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni