Ijumaa, 27 Desemba 2024

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA YA MWANZO INONELWA AFARIKI DUNIA

                                                                                TANZIA




                     Marehemu Leah Valentine Kagwidi enzi za uhai wake.


Uongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, unasikitika kutangaza  kifo cha Mtumishi wa Mahakama ya Mwanzo Inonelwa, Bi. Leah Valentine Kagwidi, aliyekuwa Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la I.

Marehemu Kagwidi alifikwa na umauti mnamo  tarehe 25 Desemba, 2024, majira ya saa 12 :00 asubuhi mara baada ya kuugua ghafla siku ya tarehe 24 Desemba, 2024. 

Aidha, Uongozi wa Mahakama hiyo unawafahamisha kwamba mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya Misungwi.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Kijiji cha Hungumalwa kilichopo Wilaya ya Kwimba.Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa kushirikiana na familia, na maziko yanatarajiwa kufanyika leo Ijumaa  tarehe 27 Desemba, 2024 nyumbani kwa marehemu Hungumalwa.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMEN.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni