Na. Hilary Lorry – Mahakama, Lindi
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi
Bi.Quip Godfrey Mbeyela amekabidhiwa majengo matatu ya Mahakama za Mwanzo
ambazo ni pamoja na Mahakama ya Mwanzo Ndomoni iliyopo Wilaya ya Nachingwea,
Mahakama ya Mwanzo Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi na Mahakama ya Mwanzo Mtandi
iliyopo Wilaya ya Kilwa zote zikiwa Mkoa wa Lindi.
Makabidhiano
hayo yalifanyika kwa siku mbili kati ya tarehe 8 na 9 Septemba 2025 ambapo tarehe
08 Septemba 2025 Mtendaji huyo alikabidhiwa Mahakama ya Mwanzo Ndomoni iliyopo
wilaya ya Nachingwea na tarehe 9 Septemba 2025 alikabidhiwa Mahakama za mwanzo
Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi na Mahakama ya
Mwanzo Mtandi iliyopo wilaya ya Kilwa.
Aidha,
zoezi la makabadhiano ya majengo hayo matutu ya Mahakama za Mwanzo yamefanyika
kati ya kampuni ya Uandisi ya Engineering Plus ambao ni wajenzi wa majengo hayo chini ya Mhandisi mshauri kutoka
kampuni ya Norman na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi.
Akizungumza
wakati wa zoezi la makabidhiano hayo Mtendaji Mbeyela aliipongeza kampuni ya
Engineering Plus kwa kufanya kazi hiyo ya ujenzi kwa weledi na ufanisi mkubwa.
“Nimpongeza
Mhandisi Mshauri na jopo lake kutoka kampuni ya Norman kwa usimamizi mzuri wa
mradi huku akiwasisitiza kuendelea kufuatilia majengo hayo kwa ukaribu wakati
wote ambapo majengo hayo yapo katika muda wa uangalizi (probation period),”
aliongeza Mtendaji huyo.
Kwa
upande, Mkadiriaji Majenzi Bw. Abdallah Nalicho kutoka Makao Makuu ya Mahakama
ya Tanzania aliwataka kampuni ya Engineering plus kutoa mafunzo juu ya mifumo
mbalimbali ikiwemo mifumo ya umeme, mifumo ya TEHAMA, Mifumo ya kuzuia na
kudhibiti moto na mifumo mingine yote ndani ya siku kumi na nne (14) tangia
kukabidhiwa miradi hiyo.lengo ni kuwafanya watumiaji wawe na uelewa mzuri wa
namna bora ya matumizi ya mifumo hiyo.
“Niwashauri
watuamiaji kuripoti dosari zozote zitakazojitokeza kwa haraka hasa wakati huu
ambapo majengo haya yapo chini ya uangalizi ili mkandarasi ajuzwe na kuweza kurekebisha
kasoro zozote zitakazojitokeza na akimtaka mhandisi mshauri kushiriki katika
kusimamia marekebisho yoyote yatakayojitokeza kwani bado ni jukumu lako kwa
kipindi hiki cha uangalizi,” alisema Bw. Nalicho.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Mhandisi kutoka kampuni ya Engineering plus Bw. Silas Paul
na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Norman Bw. Beno Batinamani waliupongeza Uongozi
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kipindi
chote jambo ambalo limefanya majengo hayo matatu ya mahakama za Mwanzo
kukamilika katika ubora uliokusudiwa.
“Jambo
moja la kutilia mkazo kwa watumiaji ni kuongeza umakini katika kutunza vifaa
vyote vilivyowekwa kwenya Mahakama hizo ili viweze kuleta tija iliyokusudiwa na
kutomuingiza yeye katika hasara ya manunuzi ya vifaa vingine hasa wakati huu
ambapo majengo yapo chini ya uangalizi,” alisisitiza Mhandisi huyo.
Jengo
jipya la Mahakama ya Mwanzo Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi linavyoonekana kwa
sasa.
Mtendaji
wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Mbeyela akipokea hati ya makabidhiano
ya majengo ya Mahakama za Mwanzo kutoka kwa Mkandarasi Mhandisi Silas Paul.
Jengo
jipya la Mahakama ya Mwanzo Ndomoni iliyopo Wilaya ya Nachingwea linavyoonekana
kwa sasa.
Wajumbe
wa kamati ya Makabidhiano wakiangalia jinsi kamera za ulinzi(CCTV CAMERA)
zinavyofanya kazi wakati wa ukaguzi wa Mahakama ya Mwanzo Mipingo.
Kaimu
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Nachingwea Mhe.Neema Mhelela akiangalia kangavuke
lililopo katika Mahakama ya Mwanzo Ndomoni.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni