.Asisitiza utekelezaji wa Maelekezo ya Mhe. Jaji Mkuu kuhusu Mahakama za Mwanzo kutokuwa na Mahabusu gerezani
Na. Kandana
Lucas- Mahakama, Musoma
Jaji Mfawidhi
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu H. Mtulya hivi karibuni, amefanya
ukaguzi wa Gereza la Wilaya ya Tarime ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa robo ya
tatu ya mwaka 2025.
Akiongea na
Mahabusu na Wafungwa wa Gereza hilo Mhe. Mtulya alieleza lengo la ziara hiyo ni
kuwapa fursa wafungwa na mahabusu kueleza changamoto zinazowakabili ili ziweze
kufanyiwa kazi na viongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na wadau wake ambao ni
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Polisi, Uhamiaji na Mawakili wa Serikali na Mawakili
wa Kujitegemea.
“Lengo la
kutembelea gereza hili ni kusikiliza changamoto za Mahabusu na Wafungwa wote
ili sisi Mahakama ya Tanzania kanda ya Musoma, tuweze kuzifanyia kazi kwa
kushirikiana na wadau wetu ambao tumeambatana nao,” alisema Jaji Mtulya.
Pamoja na
kusikiliza kero mbalimbali na kuzitolea majibu, Jaji Mtulya pia aliwasisitiza
Mahakimu wote kuendelea kutekeleza maagizo ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania
Mhe. George Mcheche Masaju kuhusu kutokuwa na Mahabusu wa Mahakama za Mwanzo
Magerezani.
Vilevile ukaguzi wa
Gereza la Wilaya Tarime, ulitanguliwa na Ukaguzi wa Mahakama za Wilaya Butiama,
Bunda, Serengeti na Tarime pamoja na Mahakama za Mwanzo Robanda Serengeti,
Nyamwaga Tarime.
Vilevile Magereza
ya Wilaya Bunda, Gereza la Kilimo na Mifugo Tabora B Serengeti na Mugumu
Serengeti ambapo Jaji Mfawidhi aliwakilishwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu
Kanda ya Musoma Mhe. Salome Abbubakar Mshasha, aliyeambatana na Mtendaji wa
Mahakama Kanda ya Musoma Bw. Leonard John Maufi.
Akimwakilisha Jaji
Mfawidhi katika Mahakama alizotembelea, Mhe Mshasha aliwahimiza watumishi
kufanya kazi kwa nidhamu, kuzingatia maadili, kusimamia vyema utaratibu wa
upokeaji na ushughulikiwaji wa malalamiko, kutokuwa na mashauri ya mlundikano,
kudumisha ushirikiano na umoja katika vituo vya kazi.
Ukaguzi huo
ulianza tarehe 17 Septemba 2025 hadi 23 Septemba 2025 ambapo Mahakama nyingine
zaidi zilizokaguliwa ni Mahakama ya Wilaya Tarime, Mahakama ya Mwanzo Tarime,
Mahakama ya Wilaya Rorya, Mahakama ya Mwanzo Ingri-Rorya, Mahakama ya Mwanzo
Nyaburongo- Rorya, Mahakama ya Wilaya Musoma, Mahakama ya Mwanzo Mukendo,
Mahakama ya Mwanzo Musoma Mjini, Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma na Gereza la
Wilaya Musoma.
Jaji Mfawidhi Mhe. Fahamu H. Mtulya (Katikati) akiwa
na Mahakimu na wadau mbalimbali wa Mahakama baada ya ukaguzi wa Gereza la
Wilaya Tarime.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma Mhe.
Salome A. Mshasha (Katikati) akiwa na Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma Bw.
Leonard J. Maufi (kulia), Mkuu wa Gereza la Wilaya Bunda Fredrick Mpokwa (kushoto)
pamoja na watumishi wa Mahakama na wadau wengine wa Mahakama (mstari wa nyuma).
Mtendaji wa Mahakama Kanda ya Musoma Bw. Leonard John
Maufi akisikiliza maelezo ya Mhandisi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo
Mugumu Mjini wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mahakama na Magereza iliyofanyika
hivi karibuni.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Mhe.
Salome A. Mshasha (Katikati) akiwa na Mtendaji Mahakimu na wadau wa Mahakama
baada ya ukaguzi wa Gereza la Mahabusu na Wafungwa Bunda
Uzio wa Mahakama ya Mwanzo Robanda- Serengeti ambao ni miongoni mwa miradi iliyokaguliwa na Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma wakimwakilisha Jaji Mfawidhi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Mhe.
Fahamu H. Mtulya (kulia), akiwa na Kaimu Mkuu wa Gereza la Wilaya Tarime SSP
Sebastian A. Dioniz (kushoto) nje ya Gereza hilo wakati wa ukaguzi.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni