Jumatano, 10 Septemba 2025

TIMU YA MAHAKAMA KAMBA WANAWAKE YAWAVUA UBINGWA UCHUKUZI

  • Wapigwa na butwaa baada ya kugalagazwa vibaya

Na EUNICE LUGIANA-Mahakama, Mwanza

Timu yay a Mahakama ya Tanzania [Mahakama Sports] Kamba Wanawake leo tarehe 10 Septemba, 2025 imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kumvuta bingwa mtetezi, Timu ya Uchukuzi kwa mvuto mmoja kwenye mchezo mkali uliokuwa wa vuta ni kuvute.

Katika mvuto wa kwanza, timu hizo zilitoshana nguvu, hivyo mshindi kupatikana kupitia mvuto wa pili na kuifanya Timu ya Mahakama kuwavuta Uchukuzi ambao wamekua mabingwa kwa miaka mitatu mfululizo.

Akiongea baada ya mchezo huo, Mhamasishaji wa Kamba Wanawake Martine Mushi amesema kamba ya Mahakama na Uchukuzi ilikuwa ngumu

"Uchukuzi wametuzoea kupiga kasia, lakini leo tumeingia na utulivu na mara wao wakivuta na sisi tunavuta, mwisho wakachoka tukawaondoa " amesema.

Naye Nahodha wa Timu hiyo, Stephania Bishobe amesema, "Kamba ilikua ngumu. tumetoka na ushindi japo kulikua na vuta nikuvute. Tunamshukuru Mungu tumepambana na tumetoka na ushindi." 

 

Timu ya Mahakama Kamba Wanawake baada ya ushindi mnono wa kuingia nusu fainali.

Timu ya Mahakama Kamba Wanawake na Wanaume pamoja na makocha wakiwa katika picha baada ya Kamba Wanawake kuingia nusu fainali.

Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Arusha

 

  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni