- Wapigwa na butwaa baada ya kugalagazwa vibaya
Na
EUNICE LUGIANA-Mahakama, Mwanza
Timu yay a
Mahakama ya Tanzania [Mahakama Sports] Kamba Wanawake leo tarehe 10 Septemba,
2025 imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kumvuta bingwa mtetezi, Timu ya Uchukuzi
kwa mvuto mmoja kwenye mchezo mkali uliokuwa wa vuta ni kuvute.
Katika
mvuto wa kwanza, timu hizo zilitoshana nguvu, hivyo mshindi kupatikana kupitia
mvuto wa pili na kuifanya Timu ya Mahakama kuwavuta Uchukuzi ambao wamekua mabingwa
kwa miaka mitatu mfululizo.
Akiongea
baada ya mchezo huo, Mhamasishaji wa Kamba Wanawake Martine Mushi amesema kamba
ya Mahakama na Uchukuzi ilikuwa ngumu
"Uchukuzi
wametuzoea kupiga kasia, lakini leo tumeingia na utulivu na mara wao wakivuta na
sisi tunavuta, mwisho wakachoka tukawaondoa " amesema.
Naye Nahodha
wa Timu hiyo, Stephania Bishobe amesema, "Kamba ilikua ngumu. tumetoka na ushindi
japo kulikua na vuta nikuvute. Tunamshukuru Mungu tumepambana na tumetoka na
ushindi."
Timu ya Mahakama Kamba Wanawake baada ya ushindi mnono wa kuingia nusu fainali.
Timu ya Mahakama
Kamba Wanawake na Wanaume pamoja na makocha wakiwa katika picha baada ya Kamba Wanawake
kuingia nusu fainali.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Arusha


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni