- Jaji Mansoor, Siyani waongoza ujumbe watu 19 kushiriki mkutano wa kimataifa
- Mahakama ya Tanzania yachomoza tena uwasilishaji mada.
Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, akifuatilia Mkutano kutoka
mbali Dodoma
Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye pia ni Makamu wa
Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. Latifa Mansoor, pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Dkt. Mustafa Mohamed
Siyani, wapo nchini Gambia kuongoza ujumbe wa watu 19
wanaoshiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Jumuiya ya Madola unaofanyika
jijini Banjul.
Mkutano huo wa 20 unaofanyika mwaka huu wa 2025, the 20th Commonwealth
Magistrates’ and Judges Association (CMJA) 2025 Annual Meeting, ulianza tarehe 21 Septemba, 2025 na utamalizika terehe 26
Septemba, 2025. Mkutano huo umehudhuriwa na jumla ya nchi 43 za Jumuiya ya
Madola.
Rais wa Gambia, Mhe. Adama Barrow, alifungua Mkutano huo
na katika hotuba, pamoja na mambo mengine, aliwakaribisha wanachama wote na kuishukuru
CMJA kwa kuamua kufanya mkutano huo mkubwa nchini kwake.
Alieleza pia namna nchi yake inavyotekeleza demokrasia,
utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu, na kwamba nchi yake
inajitahidi kwa kadri inavyowezekana kuwezesha Mahakama nchini kwake kuendana
na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Gambia, kwa niaba ya
Mahakama na jamii ya wanasheria wa Gambia, aliwakaribisha wanachama wote wa
CMJA na kuwashukuru pia kwa kauli mbiu ya mwaka 2025 inayoenda kwa jina la “Innovation
in Judicial Practice: Embracing change for a Better Future.”
Alieleza kwamba kauli mbiu hiyo inayoendana na uhalisia
wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, ambapo Mahakama duniani kote zinakumbana
na changamoto ya maendeleo kwenye sekta hiyo, hivyo imekuja kwa wakati muafaka kwani
inawezesha kupata uzoefu kutoka mataifa mbalimbali kuhusiana na chanagamoto
zinazoibuka kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kijamii au kijiografia.
Alisema kuwa uzoefu wa pamoja na ugunduzi unaotokana na
maenedeleo ya sayansi na teknolojia utakuwa nyenzo muhimu wa kuleta ufanisi
katika Mahakama, uwezo wa wananchi kufikia vyombo vya haki, na umma kujenga
imani kwa Mahakama na kuifanya iweze kwenda sambamba na maendeleo ya sayansi na
teknolojia bila kuathiri miiko, tamaduni na maadili ya kimahakama.
Katika
Mkutano huo, yupo pia Jaji
kiongozi wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yohane Masara, ambaye ameonesha ushirikiano wa
kikanda na Makamu wa Rais wa CMJA Kanda ya Kati
na Kusini mwa Afrika,ambaye pia ni Jaji
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta.
Wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Adam
Mambi, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha na
Mhe. Sharmillah Sarwat. Uwakilishi
huo
umeshirikisha pia Viongozi Waandamizi, akiwemo Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,
Mhe. Eva Nkya na Rais wa JMAT,
Mhe. Elimo Massawe.
Wengine ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
na Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Aidan Mwilapa, Mhe. Maria Mrio, Mhe. Kifungu Mrisho, Mhe.
Teddy Mlimba, Mhe. Mary Kallomo, Mhe. Devotha Kasebele, Mhe. James Mniko, na
Mhe. Fratern Temba.
Kadhalika, uwakilishi wa Mahakama kutoka Tanzania unajumuisha wajumbe wawili kutoka
Chama cha Maofisa
wa Mahkama Zanzibar (ZAJOA), Mhe.
Mohamed Sheni na Mhe. Muumin Kombo, wote Majaji wa Mahkama Kuu Zanzibar.
Wajumbe
hao walitumia fursa hii kubadilishana
mawazo na wenzao kutoka mataifa mbalimbali, kuimarisha ujuzi, na kujadili
mikakati ya kuboresha utoaji wa haki. Uwepo
w mkutano
huo unathibitisha
umoja na mshikamano kati ya vyama hivi viwili, ukihamasisha ushirikiano wa
kudumu kwa maslahi ya mfumo wa kisheria wa Tanzania.
Tofauti na hotuba mbalimbali za Viongozi, jumla ya mada 21
zitawasilishwa na kujadiliwa. Mada
hizo ni; “Innovation in Judicial Practice: Embracing Change for a better
Future”, “More efficiency or more stress: Modern Technology in the Court Room?”
na “A comparison of sentencing guidelines-do they help in sentencing or fetter
judicial discretion?”,
Nyingine ni “Artificial Intelligence- Can judges
effectively monitor its ethical use in the courtroom? “Innovation in Commercial
Courts Procedures”, “Progress on the Commonwealth Military Justice
Transformation Project’’, “Innovation to Procedures in Small claims Courts”,
“Is it no longer possible to make innovations in longstanding religious and
customary courts?” na “Innovations in Election Petition Courts”.
Mada nyingine ni “Innovations in labour/Industrial
Courts”, “Economic and Financial Crimes in the digital
Era and making criminals pay”, “Innovation in family courts
procedures", “a fireside chat”, “The Nauru Declaration on Judicial
wellbeing”, “New guidelines for appointments to Apex Courts”, “Do disciplinary
hearing for Judicial Officers pass the test of fairness?”.
Pia kuna mada zinazohusu, “Preparing for retirement”,
“Innovations by diverting female and youths from custody and the wider impact
on society”, “Social media and the judiciary-is it used
to hold us in to account or to attack us with no right to reply?”,
“Innovations in judicial procedures and cooperation in international courts”, na “What kind of protections do the judiciary
really need?”.
Wakati wa Mkutano huo, Mahakama ya Tanzania imepata
heshima ya Wataalam wawili, ambao wamebobea kwenye maeneo mbambali, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt Adam Mambi mbaye ni Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania na Mhe. Mary Kallomo, ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Mahakama ya Wilaya Morogoro, kuwasilisha mada.
Mhe. Dkt. Mambi ametoa mada ya “Economic and Financial Crimes in the digital Era and making criminals pay”, huku Mhe. Kallomo akiwasilisha mada inayohusu “Social media and the judiciary-is it used to hold us in to account or to attack us with no right to reply”.
Katika mada yake, Jaji Mambi alielezea namna uhalifu
unavyofanywa kwa njia ya mtandao wakati huu wa maendeleo ya sayansi na
teknolojia. Alieleza namna ambavyo wahalifu wanavyotumia teknolojia kufanya
uhalifu ili kuepuka nikono ya kisheria.
Alitoa mifano kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu
kuonesha namna baadhi ya wahalifu walivyoweza kufanya uhalifu kwa njia ya
mtandao na ilivyokuwa vigumu kuwapata, maana haikuwa rahisi kuweza kujua ni
sehemu gani hasa mhalifu alikuwa wakati anafanya uhalifu.
Anaeleza kuwa mawasiliano ya mhalifu huyo huonesha
mzunguko katika nchi tofauti tofati na mabara tofauti, japo baadaye huweza
kupatikana. Hivyo, alizishauri Mahakama kuendelea kujiimarisha katika
teknolojia ili kuweza kuendana na matakwa ya maendeleo ya sayansi na
teknololojia ili kukabilia na uhalifu unatendeka kimtandao hasa katika zama
hizi za sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake, Mhe. Kalomo alielezea changamoto za
matumuzi ya mitandao inavyoweza kuathiri imani ya wananchi kwa Mahakama.
Ameeleza namna Mahakama ya Tanzania ilivyoweka mikakati ya kujenga imani ya umma kupitia mageuzi ya
kidijitali kwa kusajili na kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao, sera za
uwazi, huduma kwa mteja na programe za kuelimisha jamii juu ya huduma za Mahakama.
Pia alipendekeza sera za miongozo za matumizi ya kijamii
zitengenezwe, vitengo vya kufuatilia na kujibu taarifa potofu, elimu kwa umma,
mafunzo ya maadili ya kidijitali kwa watumishi wa Mahakama na mikakati ya
kitaasisi kukabiliana na chamgamoto za kidijitali bila kuathiri uhuru wa Mahakama na kujengeana hali ya ustahimilivu wa kitaasisi na kukubali
mabadiliko.
Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, Mhe. Aisha Ally Sinda naye ni
miongoni mwa watoa mada, yeye anatarajiwa kutoa mada katika eneo la “What kind
of Protection do the Judiciary really need?” na kwakuwa hakuweza kufika
kutokana na majukumu mbalimbali, atawasilisha mada yake kwa njia ya mtandao.









Hakuna maoni:
Chapisha Maoni