Na EUNICE LUGIANA, Mahakama-Pwani
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Pwani, Mhe. Joyce Mkhoi amewataka Wakristo na Waislam kuwa wamoja maana hata vitabu vya Mungu vinasema watu wote ni sawa.
Mhe. Mkhoi aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani.
Amesema hata wakiangalia kwa sasa, Waislamu wamefunga na Wakristo nao wako Kwaresma, ameeleza, “hii haitokei kwa bahati mbaya ni jinsi tu Mungu anavyoendela kutuonesha kuwa, sisi ni kitu kimoja tunatakiwa kuishi kwa kupendana, kushirikiana lakini pia tudumishe ushirikiano kama ambavyo vile tumeweza kuyadumisha.”
Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Ustadhi Mohamed alisema, kuna watu kila siku kazi zao kuingiza huzuni kwenye mioyo ya wenzao, huku akimpongeza Mhe. Mkhoi kwa kuandaa kitu cha kuwakutaniasha watu.
“Katika mkusanyiko huu kuna watu inawezekana walikuwa na tofauti zao lakini kupitia mkusanyiko huu inawezekana tofauti zao zikaisha lakini pia kupitia mkusanyiko huu tunaweza kupata marafiki wengi watu wakabadilishana mawasiliano lakini mwisho wa siku wakatengeneza amani zaidi na upendo na mshikamano kwa sababu tu iliyosababishwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani,” amesisitiza Ustadhi Mohamed.
Iftar hiyo iliyoandaliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani iliwajumuisha watumishi wa Mahakama ya Wilaya Kibaha na Mahakama ya Wilaya Kisarawe.
Sehemu ya watumishi na waalikwa katika hafla ya iftar iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani.
(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Mwanza)
.jpg)




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni