Ijumaa, 19 Juni 2026

JAJI FAHAMU MTULYA AKABIDHIWA OFISI MAHAKAMA KUU MASJALA NDOGO MBEYA

Na. MUKSINI NAKUVAMBA – Mahakama, Mbeya

Aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga, tarehe 17 Juni, 2026 alimkabidhi rasmi Ofisi Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya baada ya kuripoti katika kituo chake hicho kipya cha kazi.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mhe. Tiganga alitoa shukrani zake za dhati kwa viongozi na watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya na kumpongeza Mhe. Mtulya kwa kukabidhiwa majukumu hayo na kumtakia heri na mafanikio katika utekelezaji wa majukumu ya kuiongoza Masjala hiyo ya Mbeya.

Hafla hiyo ya makabidhiano ya Ofisi ilifanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, ikihudhuriwa na aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga, Jaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti na Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Wilaya Mkoa wa Mbeya.

Makabidhiano hayo yalijikita katika kukabidhi majukumu ya kiutawala, nyaraka mbalimbali za ofisi, na taarifa muhimu za utendaji kazi, zote zikiwa na lengo la kuhakikisha mwendelezo wa utoaji wa huduma za kimahakama na usimamizi wa shughuli za Mahakama katika Masjala Ndogo ya Mbeya.

Kwa upande wake, Mhe. Mtulya aliahidi kuendesha ofisi hiyo kwa weledi, kuendeleza ushirikiano baina ya watumishi na kuimarisha upatikanaji wa huduma za haki kwa wananchi wanaotumia Masjala hiyo ya Mbeya.

Makabidhiano hayo yanaashiria mwanzo wa awamu mpya ya uongozi katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya, huku yakisisitiza dhamira ya kuendeleza ufanisi, uwazi na ubora katika utoaji wa huduma za Mahakama kwa wananchi.

Jaji Mfawidhi mpya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, (kushoto) na aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (kulia) wakikabidhiana Ofisi katika kituo cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.

Jaji Mfawidhi mpya Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya, (kushoto) na aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) wakisaini nyaraka za makabidhiano ya Ofisi na kulia ni Jaji waMahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Mussa Pomo akishuhudia kitendo hicho.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya katika hafla hiyo 

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (kulia) akimpa kipande cha keki Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (kushoto) ikiwa ni ishara ya kumkaribisha.



Sehemu ya watumishi walioshiriki katika  katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Ofisi

Sehemu ya watumishi walioshiriki katika  katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Ofisi

Aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (katikati) akikabidhiwa zawadi na Mtendaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Bi. Mavis Miti (kushoto).

Aliyekuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga akikata keki ya kuagwa katika hafla hiyo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya akikata keki ya ukaribisho katika hafla hiyo.

Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akipokelewa na Viongozi na watumishi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Mbeya.

(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni