Jumanne, 16 Agosti 2016

MHE. JAJI KIONGOZI ATEMBELEA MAHAKAMA KUU KANDA YA MOSHI

 Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu alipowasili mapema tarehe. 16.08.2016 kujionea hali ya utoaji haki katika Kanda hiyo. Aliyepo nyuma ya Mhe. Jaji Kiongozi ni Mhe. Aishieli Sumari, Jaji Mfawidhi , Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, anayefuata nyuma ya Mhe. Sumari ni Mhe. Mpepo, Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, nyuma yake ni Mhe. Fatuma Massengi, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
Mhe. Ferdinand Wambali, Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania akisaini kitabu cha wageni pindi alipowasili Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi kwa ziara ya kikazi, aliyeketi ni Mhe. Benedict Mwingwa, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi. (mwenye koti la draft).
Mhe. Jaji Kiongozi akiendelea kuwasalimia watumishi wa Mahakama, Kanda ya Moshi.
Mhe. Jaji Kiongozi akisalimia na baadhi ya Mawakili wa Kanda ya Moshi waliowasili kumpokea katika Viwanja vya Mahakama Kuu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni