Alhamisi, 18 Agosti 2016

WATUMISHI WA MAHAKAMA KUU-MASJALA KUU DAR ES SALAAM WAPATIWA MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Moses Mzuna akifungua rasmi mafunzo ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Mahakama ya Tanzania, 2015/2016-2019/2020 kwa watumishi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanalenga katika kuwajengea uelewa wananchi juu ya mambo muhimu ya kuzingatia katika utekelezaji. Aliyeketi ni Bw. Sollanus Nyimbi, Mtendaji, Mahakama Kuu ya Tanzania.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kuu wakiwa katika Mafunzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama, mafunzo hayo ya Mpango Mkakati yalitolewa pia Mahakama ya Kazi, Mahakama ya Ardhi na Mahakama ya Biashara na yataendelea kufanyika kwa Mahakama zingine za Dar es Salaam.
 Mhe. Mustapha Siyani, Naibu Msajili, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akitoa somo kwa watumishi wa Mahakama Kuu juu ya Mpango Mkakati wa Mahakama.
Mtendaji, anayeshughulia Mahakama Kuu-Masjala Kuu, Bw. Samson Mashalla akitoa somo kwa Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika mafunzo hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni