Jumanne, 11 Juni 2024

JAJI MNYUKWA AFUNGUA MAFUNZO KUHUSU KANUNI ZA UPOKEAJI WA USHAHIDI WA KIELEKRONIKI

  Na Naomi Kitonka, Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia- Temeke

Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia,(IJC) Temeke Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa leo tarehe 11Juni, 2024 amefungua mafunzo  kuhusu kanuni za upokeaji wa ushahidi kielektroniki yenye lengo la kubadilishana uzoefu kwa mahakimu wa kituo hicho.

Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye Kituo hicho, Mhe. Jaji Mnyukwa alisema katika uendeshaji wa mashauri, kuna sehemu ya ushahidi ambayo ndiyo inatusaidia kufanya maamuzi na kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia aina za ushahidi zimeongezeka.

“Tunao wajibu wa kuhakikisha kila shauri linafikia mahali pazuri na wananchi wanapata haki hivyo mafunzo ya siku ya leo ni kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa namna gani tunaweza kupokea ushahidi huo,kupima uzito wa ushahidi huo na kufanya maamuzi sahihi,” alisema Jaji Mnyukwa.

Naye Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi akitoa elimu hiyo alisema“Tunapofanya majukumu yetu ya kuwapatia wananchi haki, ushahidi ni kitu cha muhimu sana, hivyo Sheria ya Electronic Transaction Act iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 kifungu cha 18 (1)(2) inatutaka kukubali ushahidi wa kielektroniki katika mwenendo wa shauri lolote la kisheria pasipo kuondoa uhalali wake kanuni za ushahidi zinapotumika,”. 

Aidha alisema pia uhalali wa ushahidi huo unakuwepo ili kuepuka makosa na kusababisha ukosefu wa haki kwa moja kati ya pande zinazohusika na namna ya kutunza taarifa muhimu za wadaawa.

Akifunga mafunzo hayo, Mhe. Jaji GladysNancy Barthy alimshukuru Mhe. Jaji Mambi kwa elimu iliyoitoa na alitoa pongezi kwa Wahe. mahakimu kwa kujifunza namna ya kushughulikia ushahidi unapoletwa mahakamani, huku  akisisitiza kuwa ni jukumu la wote ili kurahisisha upatikanaji wa haki katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknolojia.  

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya  Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (aliyesimama katikati) akitoa neno la ufunguzi wa mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Evodia Kyaruzi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi (aliyekaa wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Sharmilla Sarwatt (aliyekaa wa pili kulia), na Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Watoto, Mhe. Vicky Mwaikambo (aliyekaa wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya  Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (aliyekaa Katikati), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi (aliyekaa wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. GladysNancy Barthy (aliyekaa wa pili kulia), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Evodia Kyaruzi (aliyekaa wa kwanza Kushoto) na Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Watoto Mhe. Vicky Mwaikambo (aliyekaa wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja.


Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi akitoa wasilisho kwa wahe. mahakimu waliohudhuria katika mafunzo hayo katika Kituo cha IJC Temeke. 


Jaji wa Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Masuala ya FamiliaTemeke, Mhe. GladysNancy Barthy akitoa neno la shukrani katika mafunzo hayo.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya  Familia Temeke, Mhe. Mnyukwa (aliyekaa katikati), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi (aliyekaa wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. GladysNancy Barthy (aliyekaa wa pili kulia), NaibuMsajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Evodia Kyaruzi (aliyekaa wa kwanza Kushoto) na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Watoto Mhe. Vicky Mwaikambo (aliyekaa wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mahakimu waliohudhuria mafunzo, Kituo cha IJC Temeke.

Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya  Familia Temeke, Mhe. Mwanabaraka Mnyukwa (aliyekaa katikati), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi (aliyekaa wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. GladysNancy Barthy (aliyekaa wa pili kulia), NaibuMsajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Evodia Kyaruzi (aliyekaa wa kwanza Kushoto) na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Watoto Mhe. Vicky Mwaikambo (aliyekaa wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mahakimu waliohudhuria mafunzo, Kituo cha IJC Temeke.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni