Na Iman Mzumbwe-Mahakama, Mbeya
Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda Mbeya ilifanya hafla ya kuwaaga viongozi wanne waliohama
na kuwakaribisha viongozi wengine watano waliohamia Mahakama Kuu, Kanda hiyo
wakiwemo Majaji watatu, Naibu Msajili mmoja (1) na Mtendaji wa Mahakama Kuu.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Dunstan Ndunguru akiongoza
hafla hiyo mwanana aliwakaribisha wageni waalikwa, wadau wa Mahakama, watumishi
waliohama pamoja na wale waliohamia Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
Vilevile
Mhe. Ndunguru aliwashukuru Viongozi wote kwa kujitoa kwao wakati wote
walipokuwa wanatekeleza majukumu yao na kuwapongeza viongozi hao kwa kutenga
muda wao adhimu kuitikia wito wa kufika katika hafla hiyo ili kuwaaga rasmi.
“Haikuwa
rahisi sana kuacha majukumu yenu ya msingi ya kuwahudumia wananchi na kutenga
japo muda kidogo mkafika hapa kwa ajili ya jambo dogo kama hili hakika
mmetuheshimisha kwa kuwa nasi hapa leo hii, tumefurahi kukutana nanyi
wanafamilia wenzetu,” alisema Jaji Ndunguru.
Mhe,
Dunstan Ndunguru aliwaeleza viongozi hao kwamba licha ya kuwaaga bado Mahakama
Kuu Kanda ya Mbeya ni nyumbani kwao, hivyo aliwasisitiza kwamba wanapopata
nafasi wasisite kufika ili wasalimie na kubadilishana mawazo na watumishi
waliopo.
Hafla
hiyo iliwajumuisha Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Waheshimiwa Naibu Wasajili,
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mahakimu Mahakama zote za Mkoa wa Mbeya
na Mkoa Songwe, watumishi wa Mahakama Mbeya na Songwe, pia wadau wa Mahakama wa
Kanda nzima ya Mbeya. Mchaparo ho ulifanyika tarehe 31 Mei, 2024 katika ukumbi
wa Beaco Resort Kadege Mbeya.
Viongozi
walioagwa ni pamoja na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. James
Karayemaha, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliyehamishiwa Mahakama Kuu, Kanda
ya Dar es slaam Mhe, David Ngunyale, Naibu Msajili Mwandamizi Mhe, Projestus Kahyoza
aliyehamia Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma
na Mtendaji wa Mahakama Kuu Bw.Teoford Ndomba aliyehamia Mahakama Kuu Kanda
ya Tabora.
Wakati
viongozi waliokaribishwa ni Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe.
Mussa Kassim Pomo, Mhe. Emmanuel Kawishe, Mhe. Aisha Sinde, Naibu Msajili Mhe. Judith
Lyimo pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Miti.
Aidha,
viongozi walioagwa walitoa shukrani zao kwa uongozi wa Mahakama Kuu, watumishi
na wadau mbalimbali waliojitokeza kuwaandalia na kushiriki hafla hiyo kwa pamoja
na kuwapa zawadi malimbali nzuri ambazo walikiri kufurahishwa nazo katika tukio
hilo.
Kwa
niaba ya viongozi walioagwa, akitoa neno hilo la shukurani Jaji Mfawidhi
Mahakama Kuu, Kanda ya Songea Mhe. James Karayemaha aliwaahidi watumishi na
wadau kuendelea kutoa ushirikiano kwa pamoja watendelea kuwa sehemu ya familia
ya Kanda ya Mbeya na kutoa msaada wa kiutendaji wakati wowote watakapo itajika
kufanya hivyo.
Katika
tukio jingine, Mhe. Ndunguru alizindua klabu ya mazoezi ya Mahakama Kuu Kanda
ya Mbeya ijulikanayo kama Mahakama Mbeya
Jogging Club na kwa kutambua ushiriki wa viongozi walioagwa wakati klabu hiyo
ilipoanzishwa.
Mhe.
Ndunguru alitumia muda huo kuwagawia vifaa vya mazoezi kama vile Jezi viongozi
walioagwa pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ambao wamekuwa wakishiriki
katika mazoezi hayo mara kwa mara. Mazoezi hayo yanyobeba kaulimbiu ijulikanayo
kama Mazoezi ni Uchumi, Afya na Ndoa
na kuwahimiza watumishi wote wa Mahakama kujiunga na klabu hiyo.
Hafla
hiyo iliambatana na ugawaji wa tuzo na zawadi mbalimbali kwa viongozi walioagwa
pamoja na watumishi wa Mahakama na wadu wa Mahakama (souvenir) kwa kufanisha hafla hiyo.
Naye,
Naibu Msajili Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu alitoa neno la
shukurani kwa niaba ya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa waalikwa kwa kuhudhulia
kwao kwani walionesha upendo na umoja zaidi na aliendelea kusisitiza umoja na
ushirikiano sehemu za kazi.
Sehemu ya Viongozi wa Mahakama waliohama Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya Viongozi wengine waliohamia Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya walipokuwa kwenye Mchaparo hafla hiyo ulifanyika tarehe 31 Mei, 2024 katika ukumbi wa Beaco Resort Kadege Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni