Na Mwandishi Wetu - IJA
Watumishi
wa Mahakama ya Tanzania wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha
wanakidhi matarajio ya Taasisi wanaposhiriki mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa
na Mahakama kwa ajili ya kuboresha na kukidhi haja ya kuongeza tija na ufanisi
katika utendaji kazi.
Wito
huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa
Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa
maafisa wapatao 15 wanaoshiriki namna bora ya kuendesha mafunzo kwa njia ya
masafa ya kielektroniki (e- Learning) yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahamaka
- Lushoto IJA kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 27 mwenzi Juni, 2024.
Bi.
Patrick alisema kuwa lengo la mafunzo hayo siyo kuwapa tu washiriki ujuzi wa
kuandaa kozi na mada za kufundishia bali ni kuwaandaa kuwa walimu na mabalozi
wa matumizi ya mfumo wa e-learning kwa watumishi wengine.
Aidha,
Bi. Patrick aliongeza kuwa, Mahakama imekuwa ikikumbana na changamoto
mbalimbali ikiwemo uhaba wa Rasilimali Fedha, muda kutokuwa rafiki wa kuwawezesha
watumishi wote kushiriki na kupata mafunzo kwa watumishi wote kwa nchi nzima. Sanjali
na hilo Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na
Mahakama ya Tanzania bado wamekuwa na uwezo wa kupata nafasi ya kuandaa baadhi
ya mafunzo ya kimkakati ili kuziba pengo la ujuzi na maarifa miongoni mwa
watumishi kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Vilevile,
Bi. Patrick alisema Mahakama kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA)
ambao ndiyo wenye dhamana ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mahakama wamefanikisha
ujenzi wa mfumo wa kufundishia kwa njia ya masafa (e-Learning) ambao
umekamilika kwa asilimia 98.
Mfumo
huo ambao utawezesha kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali
kwa lengo la kuwaongezea ujuzi katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha na
kuongeza ufanisi kwa watumishi. Mfumo huo utaweza kuwafikia watumishi wengi kwa
wakati mmoja kwa urahisi zaidi pamoja na kupanua wigo wa kuongeza washiriki
wengi zaidi na kuiwezesha Mahakama kuendesha mafunzo mbalimbali ya watumishi
kwa garama nafuu.
Kwa
upande wao, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Hakimu Mkazi Mwandamizi
wa Mahakama ya Iringa Rehema Mayagilo na Hakimu Mkazi Mkuu Mwandamizi Mhe. Richard
Kabate walisema mafunzo hayo ya matumizi ya mfumo huo yatakwenda kutoa nafuu
kubwa kwa Mahakama kuwafikia watumishi wengi kwa wakati mmoja pamoja na Chuo Uongozi
wa Mahakama Lushoto kuandaa mafunzo kwa Wanafunzi kwa njia ya kielektroniki ama
kimtandao.
Mafunzo
hayo yanashirikisha washiriki 15 miongoni mwao wapo Naibu Msajili (1) mmoja,
Mahakimu Wakazi wanane (8), Wakufunzi kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama –
Lushoto (IJA) wawili (2) Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala watatu (3) na Afisa
Habari mmoja (1).
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick akifungua mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada na Masomo ya kujifunza mafunzo mbalimbali kwa watumishi kwa njia ya Masafa (e-Learning) yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA) jana tarehe 18 Juni, 2024
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick akifungua mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada za mafunzo kwa njia ya Masafa (e-Learning) yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA) jana tarehe 18 Juni, 2024
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni