Jumatano, 19 Juni 2024

MWAROBAINI WA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA WAKARIBIA KUPATIKANA

Na Mwandishi Wetu - IJA

Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu wa kuhakikisha wanakidhi matarajio ya Taasisi wanaposhiriki mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na Mahakama kwa ajili ya kuboresha na kukidhi haja ya kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi.

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa maafisa wapatao 15 wanaoshiriki namna bora ya kuendesha mafunzo kwa njia ya masafa ya kielektroniki (e- Learning) yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahamaka - Lushoto IJA kuanzia tarehe 18 hadi tarehe 27 mwenzi Juni, 2024.

Bi. Patrick alisema kuwa lengo la mafunzo hayo siyo kuwapa tu washiriki ujuzi wa kuandaa kozi na mada za kufundishia bali ni kuwaandaa kuwa walimu na mabalozi wa matumizi ya mfumo wa e-learning kwa watumishi wengine.

Aidha, Bi. Patrick aliongeza kuwa, Mahakama imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa Rasilimali Fedha, muda kutokuwa rafiki wa kuwawezesha watumishi wote kushiriki na kupata mafunzo kwa watumishi wote kwa nchi nzima. Sanjali na hilo Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania bado wamekuwa na uwezo wa kupata nafasi ya kuandaa baadhi ya mafunzo ya kimkakati ili kuziba pengo la ujuzi na maarifa miongoni mwa watumishi kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Vilevile, Bi. Patrick alisema Mahakama kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) ambao ndiyo wenye dhamana ya kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mahakama wamefanikisha ujenzi wa mfumo wa kufundishia kwa njia ya masafa (e-Learning) ambao umekamilika kwa asilimia 98.

Mfumo huo ambao utawezesha kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea ujuzi katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha na kuongeza ufanisi kwa watumishi. Mfumo huo utaweza kuwafikia watumishi wengi kwa wakati mmoja kwa urahisi zaidi pamoja na kupanua wigo wa kuongeza washiriki wengi zaidi na kuiwezesha Mahakama kuendesha mafunzo mbalimbali ya watumishi kwa garama nafuu.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Iringa Rehema Mayagilo na Hakimu Mkazi Mkuu Mwandamizi Mhe. Richard Kabate walisema mafunzo hayo ya matumizi ya mfumo huo yatakwenda kutoa nafuu kubwa kwa Mahakama kuwafikia watumishi wengi kwa wakati mmoja pamoja na Chuo Uongozi wa Mahakama Lushoto kuandaa mafunzo kwa Wanafunzi kwa njia ya kielektroniki ama kimtandao.

Mafunzo hayo yanashirikisha washiriki 15 miongoni mwao wapo Naibu Msajili (1) mmoja, Mahakimu Wakazi wanane (8), Wakufunzi kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA) wawili (2) Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala watatu (3) na Afisa Habari mmoja (1).

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick akifungua mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada na Masomo ya kujifunza mafunzo mbalimbali kwa watumishi kwa njia ya Masafa (e-Learning) yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA) jana tarehe 18 Juni, 2024

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick akifungua mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada za mafunzo kwa njia ya Masafa (e-Learning) yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA) jana tarehe 18 Juni, 2024

Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo wa Mahakama ya Tanzania Bi. Patricia Ngungulu akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada za mafunzo kwa njia ya Masafa (e-Learning) 


Sehemu ya wataamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) walioshiriki kujenga mfumo wa kufundishia kwa njia ya masafa (e-Learning) ambao umekamilika kwa asilimia 88. 


Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo wa Mahakama ya Tanzania Bi. Patricia Ngungulu akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada za mafunzo kwa njia ya Masafa (e-Learning) 

Meza Kuu ikiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bi. Beatrice Patrick (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya watumishi wanaoandaliwa kuwa wataalam wa eneo la kuandaa mada na Masomo ya mafunzo kwa njia ya Masafa (e-Learning). 





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni