Alhamisi, 6 Juni 2024

JAJI BARTHY: KUWENI MABALOZI WAZURI WA UKATILI WA KINGONO NA KIJINSIA

 Na Magreth Kinabo- Mahakama 

 

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke, Mhe. Glady’s Nancy Barthy amewasihi mahakimu waliopatiwa mafunzo ya unyanyasaji wa kingono na ukatili wa jinsia wawe mabalozi wazuri elimu hiyo kwa wengine.

 

Mafunzo hayo yaliyofanyika kituoni hapo kwa siku tatu yamefungwa  jana na Mhe. Barthy na yamehusisha mahakimu kutoka ngazi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambaye amewataka kuendelea kujifunza wenyewe elimu waliyopatiwa ili waweze kuwa wabobezi,kwa kuwa suala hilo ni endelevu.

 

“Ni utamaduni mzuri pale unapotoka kufanya mafunzo na wewe ukaenda kuwekeza na kuwafundisha wale ambao wako katika maeneo yetu ya kazi, kwa hiyo inafaa kuenda kuwafundisha wengine, na unapowafundisha wengine inakujengea uwezo na ujuzi zaidi, katika eneo ambalo unalitolea mafunzo.

 

“Ni muhimu kutambua ya kwamba jukumu la Jaji au Hakimu katika kuhakikisha anazingatia wadawa au mashahidi walio katika makundi ya maalum au yenye changamoto yanayohitaji kuangaliwa kwa upekee mfano wazee, watoto na walemavu na wale wote wanaohitaji msaada wa kipekee katika kuhakikisha kwamba haki inatendeka,”alisema Mhe. Jaji Barthy. 

 

Aliongeza kuwa upande mashauri yanayohusu watoto ni muhimu kuzingatia Sheria ya Mtoto na kanuni zake.

 

Mhe. Jaji Barthy alifafanua kuwa ni vizuri kutoa kipaumbele kwa mashauri yanayohusisha makundi hayo yenye changamoto kwa kuhakikisha yanamalizika ndani kwa kipindi cha miezi sita tangu yalipofunguliwa, ikiwemo kuweka mazingira rafiki wakati wanapofika  mahakamani.

 

Aidha alisema ni vema kutumia wataalamu lugha za ishara kwa mashahidi ya watu wenye ulemavu wa kutosikia au kuongea, kuhakikisha wanapata mwenendo, tuzo na amri za mbalimbali zinatolewa katika mashauri ya makundi hayo, kutoa nakala za hukumu kwa wakati, ikiwemo msaada wa kisheria pale inapobidi na kutumia kanuni tulizojifunza katika mashauri ya makundi yenye changamoto. 

 

Aliwataka kujiongoza na kufanya yale waliyofundishwa uthabiti na pia ni sambamba  kwa kuzingatia miiko ya kazi wakiwa kama maafisa  mahakama ili kujenga imani kwa jamii.

 

Alisema inapaswa kutambua mawasiliano yanayofanyika katika vyumba vya mahakama kwamba matendo yao yanaweza kuua au kuhuhisha, hivyo ni lazima kuwe na matendo ambayo yataweza kuhakikisha kwamba hisia zinalindwa na kutumia ufundi au namna mbalimbali ya kuhakikisha yale unayoweza kupata kwa shahidi anayetoka katika makundi hayo.

 

Aliushukuru uongozi wa Mahakama ya Tanzania, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Irish Rule of Law International (IRLI) kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo katika Kituo hicho.

 

Lengo   mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo mahakimu hao wa jinsi ya kuepuka kutonesha majeraha ya kisaikolojia kwa mashahidi na waathirika, hususani katika kesi za unyanyasaji wa kingono na ukatili wa kijinsia (Avoiding Re-traumatization) wanaposikiliza mashauri hayo.

 Kaimu Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke, Mhe. Glady’s Nancy Barthy (katikati)akitoa hotuba yake kufunga mafunzo ya ukatili wa kingono na kijinsia, uliofanyika jana kituoni hapo.Kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu,Mhe. Evodia Kyaruzi na kushoto ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo, Mhe. Raymond Kaswaga.
 Kaimu Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke, Mhe. Glady’s Nancy Barthy, (katikati) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Mhe. Ali Mkama.


Kaimu Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia (IJC) Temeke, Mhe. Glady’s Nancy Barthy, (katikati) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Mhe. Joyce Mkhoi.


 
 Hakimu wa Mahakama ya Watoto ya Kisutu, Mhe. Veronica Mtete akiwasilisha mada kuhusu ukatili wa kingono na  kijnsia.


 Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Watoto Kisutu,Mhe. Orupa Mtae (aliyenyoosha mkono) akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya kikundi.


 Mahakimu hao wakiwa katika vikundi vya majadiliano.



Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Mhe. Nabwike Mbaba akifafanua jambo.

 Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke,Mhe. John Ngeka akiwasilisha mada kuhusu mafunzo hayo. 


Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika mahakama ya mfano kuhusu uendeshaji wa kesi zinazohusisha ushahidi kutoka makundi yenye changamoto maalum.

Mahakimu wakisikiliza mada.

 

 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni,Mhe. Ishaq Kuppa (kushoto) na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Bittony Mwakisu wakiwasilisha mada  kuhusu mafunzo hayo.



Picha ya juu na chini ni Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu hao. 



 Meza Kuu na Sekretarieti .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni